29.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 19, 2022

Polisi: Tumetumia mbwa kumkamata anayedaiwa kuua mpenzi wake

JANETH MUSHI-ARUSHA

JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha, limeeleza namna lilivyotumia mbwa kumkamata mwimbaji wa nyimbo za injili, Mosses Pallangyo (28), anayedaiwa kumuua mke wake, Mary Mushi(24),wakati akijaribu kutorokea nchini Kenya.

Pallangyo anadaiwa kumuua mkewe ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za injili,Desemba 25, mwaka huu kwa kumkata na shoka kichwani, nyakati za  mchana katika Kijiji cha Kilinga, wilayani Arumeru.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kituo cha Poliso Usa River,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana alisema walimkamata Desemba 28, mwaka huu saa 11 jioni.

Alisema walimkamata mtuhumiwa  akiwa Kijiji cha Ilkiushin akiwa njiani kuelekea mafichoni nchini Kenya.

“Tumekuwa  Arumeru kwa siku tatu mfululizo usiku na mchana kufuatia operesheni kabambe tuliyokuwa tunafanya kumtafuta mhalifu

aliyefanya kitendo cha kinyama na kikatili ambacho hakikubaliki katika jamii iliyostaarabika.

“Mbinu tuliyotumia ni ya mbwa ambayo ni ya kunusa,bandika bandua mguu kwa mguu mpaka unamfikia, juhudi hizi zilizaa matunda baada ya mtego uliokuwa umewekwa na askari na alikamatwa akiwa njiani kuelekea

mafichoni nchini Kenya,”aliongeza

Alisema baada ya kumkamata na kumhoji kwa kina, alikiri kufanya kitendo hicho na kudai alipitiwa na shetani.

“Tulipomkamata tulienda mbali zaidi na kutaka kujua kwanini alifanya kitendo hicho,alisema ni shetani ila hili labda watu wa imani watatusaidia mimi nashindwa kumpeleleza shetani.

“Kutokana na tukio hili, nandelee kuwaomba wananchi kitendo cha kujichukulia sheria mkononi kutoa uhai wa mtu mwingine kwa namna au sababu yoyote kamwe hazitakubalika,”alisema.

Inaelezwa  mtuhumiwa na marehemu, walianza kuishi wiki tatu zilizopita, ambapo wakati Pallangyo akikamatwa taarifa zinadai vikao vya familia baina ya pande zote mbili vinaendelea baada ya upande wa marehemu kutaka mahari ilipwe kwanza ndipo wazike.

Taarifa zinasema Pallangyo hakuwahi kulipa mahali ya kuishi na Mary na kwa mujibu wa familia kwa taratibu zao, licha ya tukio hilo la mauaji kutokea, mahari ilipwe kwanza ndipo azikwe.

mlezi wa waimbaji wa nyimbo za injili nchini, Emanuel Mbasha alisema wamesikitishwa na kuumizwa na tukio hilo na kuwa baada

ya kutokea kulikuwa na tarmharuki kila mmoja akizungumza jambo lake ila wanashukuru Jeshi hilo kumkamata mtuhumiwa.

Kwa upande wake, Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania(TAMUFO),Dk.Donald Kisanga alisema licha ya tukio hilo kusababisha majonzi, wanalipongeza jeshi hilo kwa kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa na kuwa wanasubiri

taratibu za kisheria zinazofuata.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,987FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles