26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi Tanga wazuia mkutano wa Zitto

AMINA OMARI Na OSCAR ASSENGA

JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga  limezuia mkutano wa ndani wa Kiongozi wa Chama wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe wa uzinduzi wa matawi kutokana na kuwapo   vurugu.

Hatua hiyo ilitokana na taarifa za  intelijensia ambazo zilidai kutokea  a vurugu ambazo ziliratibiwa na wanachama na wafuasi wa Chama cha CUF.

Akizungumza hali hiyo jana, Kiongozi wa   ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, alisema  a vitendo vinavyofanywa na vyombo vya dola vya kuzuia shughuli za chama hicho vinaonyesha namna ambavyo kinavyohofiwa kwa kuwa na nguvu kubwa kwa umma.

Alisema zuio hilo linaonyesha namna wanavyoingizwa kwenye mitego ya wanachama wao waonekane wanafanya vurugu.

Ziito alidai   kumekuwa na mazuio ya kila mara kwa chama hicho  i kinapojaribu kufanya shughuli zake kama vile mikutano ya ndani ya kuimarisha uhai wa chama .

“Hii siyo mara ya kwanza kuzuia mikutano yetu, siku chache polisi walituzuia kule Dar es Salaam na leo (jana) wamerudia hapa Tanga, hali hii nyie wananchi mnaona namna ambavyo dola inaogopa  chama chetu,” alisema Zitto.

Alidai   vyombo hivyo vimekuwa vikifuata maagizo ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ya kuwa chama hicho hakiruhusiwi kufanya mikutano yake licha ya kujaribu kuzungumza na vyombo hivyo.

Hata hivyo kiongozi huyo alishangazwa na jeshi hilo kuruhusu vyama vingine kama CUF na CCM kuendelea kufanya mikutano ya ndani na hadhara bila ya vizuizi vya aina yoyote ile.

Alisema   mpaka jana Jeshi la Polisi Wilaya ya Tanga, lilikuwa limetoa kibali kwa chama hicho kuendelea kufanya shughuli zake ikiwamo kupokea wanachama wapya na mikutano ya ndani kabla ya kuzuio shughuli hizo.

Akizungumzia hali zuio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe, alisema   taarifa za  intelejensia zinaonyesha   iwapo chama hicho kitaruhusiwa kufanya shughuli zake kunaweza kutokea uvunjifu wa amani.

Alisema   kutokana na uchunguzi wao walibaini  baada ya kuwapo   mivutano ya  siasa baina ya chama hicho na CUF  kutokana na kunyang’anyana ofisi na kuharibu baadhi ya thamani za ofisi hizo jambo linaloweza kusababisha kutokea   vurugu na amani kutoweka.

“Hivyo mazingira hayo unaona namna ambavyo wanachama wa CUF wasingeweza kukubali ACT-Wazalendo waweze kufanya shughuli zake bila ya kutokea vurugu za kulipiza kisasi.

“Tukaona ili kuepusha hali hiyo ni bora wasifanye shughuli zao walizokuwa wameomba kuzifanya,” alisema Kamanda Bukombe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles