25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi Simiyu wajivunia kupunguza makosa ya jinai

Na Derick Milton, Simiyu

Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limesema katika kipindi cha mwaka 2020 limefanikiwa kupunguza matukio ya makosa ya jinai kwa kiwango kikubwa ambapo yamepungua kutoka 7,995 mwaka 2019 hadi makosa 7,571 mwaka 2020.

Hayo yamesemwa leo Februari 6, 2021 na Kamanda wa Polisi Mkoa, ACP Richard Abwao, kwenye hafla ya siku ya polisi na familia iliyowahusisha wadau wa ulinzi na usalama Mkoa, maafisa, wakaguzi na Askari wa jeshi hilo.

Kamanda Abwao amesema kuwa kupungua kwa makosa hayo imetokana na ushirikiano mzuri kutoka kwa jamii na wadau mbalimbali katika kuhakikisha wanapinga vita matukio ya uhalifu katika maeneo yao.

“Kiwango hiki cha makosa ya jinai kupungua, ni kwa asilimia 5.3, mafanikio haya yanatokana na wadau mbalimbali na jamii kwa ujumla kutuunga mkono katika mapambano ya kuzuia uhalifu lakini pia kutoa elimu ya mara kwa Mara,” amesema Abwao.

Aidha, Kamanda huyo amebainisha kuwa jeshi hilo limejipanga kuhakikisha matukio ya makosa ya jinai yanaendelea kupungua zaidi ya hapo, huku wakitegemea zaidi ushirikiano kutoka kwa jamii na wadau wa uhalifu katika mkoa huo.

Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Tawala Msaidizi (Miundombinu), Mhandisi Mashaka Luhamba aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa amelitaka jeshi kuongeza mbinu zaidi za kupambana na uhalifu wa mitandaoni.

Mhandisi Luhamba amesema kuwa uhalifu mkubwa uliopo kwa sasa, upo mitandaoni hivyo amelitaka jeshi hilo kujifunza mbinu nyingi zaidi katika kuhakikisha wanapanga kudhibiti uhalifu huo.

Aidha, amelipomgeza jeshi hilo kwa kupunguza matukio mengi ya makosa ya jinai, ikiwa pamoja na kulinda usalama wakati wa kipindi cha uchaguzi mkuu mwaka Jana ambao ulimalizika kwa amani na usalama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles