24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi Marekani akutwa na hatia mauaji ya George Floyd

-Marekani

Afisa wa zamani wa jeshi la polisi nchini marekani, Derek Chauvin amekutwa na hatia kufuatiwa kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd huko Minneapolis mwaka jana.

Derek Chauvin mwenye umri wa miaka 45, alinaswa katika kanda ya video akipiga goti kwenye Shingo ya Floyd kwa zaidi ya dakika tisa alipokamatwa mwezi Mei mwaka uliopita.

Video hiyo iliyoibua hisia kali na kusababisha maaandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi kote duniani na utumiaji wa nguvu kupita kiasi unaofanywa na kikosi cha polisi.

Chauvin alipatikana na makosa matatu ya mauaji ya kiwango cha pili, kiwango cha tatu na mauaji bila kukusudia pia atasalia kizuizini hadi atakapohukumiwa na huenda akafungwa jela kwa miongo kadhaa.

Jopo la majaji 12 lilichukua chini ya siku moja kufikia uamuzi huo baada ya pande zote kutoa kauli zao za mwisho siku ya Jumatatu, majaji walijitenga katika hoteli kujadili kwa makini uamuzi wao.

Uamuzi huo ulishangiliwa kwa furaha nje ya mahakama, ambako mamia ya watu walikuwa wamejitokeza kufuatilia tangazo hilo.

Wakili wa familia ya Floyd, Ben Crump, alisema ni hatua ya muhimu katika historia ya Marekani.

Rais wa Marekani, Joe Biden na makamu wake Kamala Harris walipiga simu kwa familia ya Floyd mara baada ya uamuzi huo.

“Tutaongeza juhudi kuhakikisha mengine yanafikiwa hii itakuwa hatua ya kwanza muhimu ya kukabiliana na ubaguzi wa rangi uliokithiri katika mifumo yetu,” alisema Rais Biden.

Na katika hotuba ya kitaifa iliyopeperushwa kwenye runinga, Rais Biden alisema: “Ubaguzi wa kimfumo ni doa kwa roho ya taifa lote”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles