23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi kuweka vituo maalumu ufukweni

kova-July29-2014NA KOKU DAVID, DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema litaimarisha ulinzi kwa kuweka vituo vya muda katika fukwe za Bahari ya Hindi pamoja na maeneo yote yatakayokuwa na mikusanyiko ya watu wengi wakati wa mkesha wa Mwaka Mpya.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, alisema watashirikisha wadau wengine wa ulinzi na usalama ili kuhakikisha hali ya usalama inaimarika.

Alisema wakati wa mkesha wataweka ulinzi katika nyumba zote za ibada na kwamba sambamba na hatua hiyo, vikosi vyote vya polisi vitakuwa barabarani vikifanya doria saa sita kabla ya mwaka mpya.

“Tumekusudia kuwashirikisha wadau wengine wa ulinzi na usalama likiwamo Jeshi la Zimamoto, kampuni binafsi za ulinzi, wadau wanaohusika na uokoaji wakati wa majanga, vikundi vya ulinzi shirikishi, kamati za ulinzi na usalama katika ngazi zote pamoja na wakaguzi wa tarafa na askari kata kuhakikisha maeneo yote yanalindwa saa 24,” alisema Kamanda Kova.

Aidha Kamanda Kova aliwataka wafanyabiashara mbalimbali, hasa wale wa maduka ya kubadilishia fedha  na wenye maduka makubwa, kuchukua tahadhari kwa kutosafirisha fedha nyingi ikiwa ni pamoja na wananchi kutoa taarifa pale wanapoona dalili zozote au maandalizi ya uvunjifu wa amani.

Aliwataka pia madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kutoendesha vyombo vya moto kwa mwendo wa kasi ikiwa ni pamoja na kutokunywa pombe.

Katika hatua nyingine, Kamanda Kova alisema polisi wamekamata bastola moja ya Rivolver yenye namba 801340 rangi nyeusi iliyotengenezwa Brazil ikiwa na risasi mbili.

Bastola hiyo ilikamatwa Alhamisi iliyopita eneo la Ubungo Kibo wakati askari wa upelelezi walipokuwa wakifuatilia matukio ya uhalifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles