31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI KUMHOJI GRACE MUGABE


HARARE, ZIMBABWE  |

JESHI la Polisi nchini Zimbabwe limeanza uchunguzi wa biashara haramu ya meno ya tembo ambayo inamhusisha mke wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe, Grace, ambaye anatarajiwa kuhojiwa siku chache zijazo.

Kwa mujibu wa Gazeti la Serikali la The Herald, utaratibu wa kumhoji Grace Mugabe, ambaye anatuhumiwa kupanga njama za kusafirisha meno hayo kupitia meli kwenda nje ya nchi, unaandaliwa.

The Herald, ambalo lilikuwa sauti ya serikali ya Mugabe, limesema Jeshi la Polisi nchini humo limefikia hatua nzuri katika uchunguzi wake dhidi ya nafasi ya Grace Mugabe kuhusika na biashara ya meno ya tembo kwenda nchi za China, Falme za Kiarabu na Marekani.

“Jalada la uchunguzi wake linatarajiwa kufungwa siku za hivi karibuni. Tumewahi kuwakamata na kuwahoji baadhi ya watuhumiwa ambao tunaamini wanahusika na biashara hii,” kilisema chanzo cha habari kutoka Polisi.

Grace anatuhumiwa kushinikiza maofisa wa serikali kuwapa vibali vya kusafirisha meno ya tembo yenye thamani ya mamilioni ya dola kama zawadi kwa viongozi wa nchi za kigeni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles