21.4 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi Kagera yakamata watuhumiwa meno ya Tembo

Renatha Kipaka, Bukoba

JESHI la Polisi mkoani Kagera, limewakamata watuhumiwa wanne wakiwa na meno ya tembo vipande viwili vyenye uzito wa kg 0.5 na magego 28.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Awadhi Juma amethibitisha tukio hilo na kusema kwamba Novemba 18, 2021 majira ya 7:00 mchana Kata ya Nkwenda Wilaya ya Kyerwa walikamata gari aina ya ‘hiace’ yenye namba za usajili T.493DLC.

Kamanda Juma amesema gari hiyo ilikuwa ikiendeshwa na dereva,  Mwijuni Vicent(30) akiwa na wenzie Akabalimi Alfred(35) ,Paschal Joseph (25 ,) Tabu Cyplian(30) wote wakazi wa Isingoro wilayani humo,

Aidha amesema watuhumiwa hao walikuwa wamekodi siraha  aina ya Mark IV yenye namba S30629 inayomilikiwa kihalali na Paul Ishengoma mkazi wa Kata ya Kayanga Wilaya ya Karagwe mkoani humo.

“Siraha hii ni Mali ya Paul Ishengoma ndo imefanya uwindaji haramu na watuhumiwa wamekuwa wakiikodi kutoka kwa mmiliki huyo ikiwa na risasi 2 pamoja na maganda 2 tumewakamata wote”anasema Juma

Wakati huo huo kamanda  huyo amesema askari wakiwa doria walifanikiwa kukamkamata mtuhumiwa Rutwiga James (24)raia wa Rwanda (mfugaji)mkazi wa kijiji cha Lugera,Koribo Stephen(36)mkazi wa kijiji cha Rwamgulusi wakiwa na makosa ya kumteka nyara Rushirika Boniphace (36) mkazi wa lugela wilayani Karagwe .

Amesema baada ya kumteka walimweleza kuwa wanahitaji kiasi cha sh milioni 20 ili waweze kumwachia huru.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles