26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi Kagera wasambaratisha wafuasi wa Mdee kwa mabomu

Halima Mdee
Halima Mdee

Na Mwandishi Wetu, Kyerwa

JESHI la Polisi Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera limetumia mabomu ya machozi kutawanya wananchi waliojitokeza kumpokea Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee.

Walilazimika kutumia mabomu wakati Mdee alipokuwa anakwenda kusaini kitabu cha wageni kwenye ofisi za chama hicho.

Mbali na kutumia mabomu, jeshi hilo limezuia mikutano yote iliyokuwa ihutubiwe na Mdee jana kwa madai ya kupata taarifa za kiitelijensia kuwa hakutakuwa na usalama wa kutosha.

Taarifa ya kusitisha mikutano hiyo, ilipelekwa nyumbani kwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kyerwa, Deus Rutakyamilwa juzi saa 7 za usiku.

Tukio la wananchi kupigwa mabomu lilitokea jana saa 9:00 alasiri kwenye ofisi za Chadema zilizopo Kijiji cha Kwarukwazi.

Kabla wafuasi hao wa Chadema kutawanywa kwa mabomu, Naibu Katibu Mkuu wa Bawacha Taifa, Kunti Yusuph, alitangaza juu ya kusitishwa kwa mikutano na kueleza kuwa Mdee hataweza kuhutubia.

Kutokana na hali hiyo, aliwataka wanawake waliojitokeza wakutane katika kikao cha ndani Shule ya Sekondari Ndagala.

Pamoja na mikakati hiyo, polisi wakiongozwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), Pius Paul walianza kufyatua mabomu ya machozi tena kitendo kilichosababisha mkutano huo kutofanyika.

Rutakyamilwa alisema Oktoba 25, mwaka huu alitoa taarifa kwa polisi juu ya mikutano hiyo.

“Tulitangaza mikutano yetu mji mzima, tumepita mbele ya kituo cha polisi hawakutuzuia, lakini nashangaa ilipofika saa 7:00 usiku OCD alinipigia simu akiniomba niende kituoni nikamkatalia kwa sababu ulikuwa usiku.

“Katika hali ya kushangaza akaamua kuja mwenyewe nyumbani kwangu kuniletea zuio la mkutano,” alisema Rutakyamirwa.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

8 COMMENTS

  1. Yawezekana polisi wanafanya kazi kama hizi kwa woga tu wa “kumwaga unga” kama hawatawatia misukosuko wapinzani. Sijui itakuwaje siku chadema itakapounda serikali na jeshi la polisi kuendelea kuwa hili hili. Aidha sijui kama wanasiasa wanakumbuka kuwa hawawezi kufanya mikutano bila kuomba na kupewa kibali na mamlaka husika. Pia sijui kama mamlaka husika hazijui kuwa maandamano na mikutano ni haki ya kikatiba, au labda wanapokea amri toka sehemu au mtu fulani kuzuia harakati hizi? Sijui! Lakini kikubwa na cha maana zaidi ni kwamba demokrasia inakua vyema nchini.

  2. MIMI KAMA MTANZANIA NINAEIPENDA NCHI YANGU
    NIMESIKITISHWA NA KITENDO CHA MWENDELEZO WA
    POLICE KUENDELEA KUWEKA UADUI NA WANANCHI.
    KWA SABABU YA MANUFAA YA CHAMA TAWALA.
    NASEMA HII NI AIBU KWA CHAMA TAWALA NA
    NI JINSI GANI WAMEONA ANGUKO LAO 2015.
    Police wajichunge sana maana hata wao kuna siku ccm
    itawageuka.

  3. Ni muhimu sheria za nchi zifuatwe na wananchi pamoja na mamlaka zingine, polisi wapo kisheria kwa ajili ya kulinda raia pamoja na mali zao, ni jukumu lao kuongeza ukaribu na wananchi kama tuonavyo kwa nchi nyingine, lakini pa wananchi tuelewe ile dhana ya utii wa sheria bil shuruti, mambo hayo yakizingatiwa, itapunguza lawama dhidi ya jeshi hilo

  4. Inatakiwa polisi ifike sehemu mkue kifikra kwani mmekuwa mnakubali mno kutumiwa na chama tawala kwa maslai yao, ila nawatahadhalisha kuwa siku ikifika uma wa wananchi utakapochoka unyanyasaji mnaoufanya hamtaweza tena kuwasambaratisha na huto tubomu twenu twa machozi,watu wenyewe mnashida chungu nzima halafu mnajifanya kuwa nchi hii ya kwenu, YOU GUYZ THINK MORE.Msiwe na akili ya kushikiliwa.

  5. NI VIGUMU SANA KUZUIA DEMOKRASIA. KUZUIA WANANCHI KUPATA HAKI YAO YA KIKATIBA YA KUKUSANYIKA, KUSIKILIZA NA KUJIELEZA NI UHALIFU.
    PIA NI KUZIDI KUMPA HALIMA MDEE NA CHAMA CHAKE UMAARUFU. WANANCHI WASITISHIKE NA VITISHO VYA POLISI… HATA AFRIKA KUSINI WALIPITIA MAGUMU ZAIDI.. WALIHIMILI NA LEO HII YALE MANYANYASO YA DOLA YAMEBAKI KUWA NI HISTORIA.

  6. poleni wananchi mlioachiwa maumivu kwa kutaka kumsikiliza Mdee, vumilieni bila kukata tamaa. haki haiji bure bila kuidai kwa kuvumilia mateso ya yule aliyeishikilia haki yako kwa ubabe. siku ya ukombozi inakuja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles