29.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 19, 2022

Polisi akatwa sehemu za siri na mkewe

Na SAM BAHARI-SHINYANGA

JESHI la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Frola Adam (23) kwa tuhuma ya kumkata sehemu za siri na kitu chenye ncha kali na kumjeruhi vibaya mume wake ambaye ni askari.

Akizungumza jana mjini hapa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Deborah Magiligimba, alisema tukio hilo lilitokea Desemba 28, mwaka jana saa 6.30 usiku wakati wamelala.

Alidai siku ya tukio askari polisi H. 8980 PC Kazimir (28), akiwa amelala katika chumba chake kwenye nyumba iliyopo Mtaa wa Mitimirefu (Uzunguni), Shinyanga Mjini, ghafla mke wake alimkata na kitu chenye ncha kali katika uume wake na kumsababishia maumivu makali.

Kamanda Magiligimba alidai PC Kazimir akiwa amelala, mke wake Frola aliamka na kunyata akachukua kitu chenye ncha kali  na kisha kumkata sehemu zake za siri na kumjeruhi vibaya.

Alisema baada ya tukio hilo, PC Kazimir alikimbizwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga ambako alilazwa kwa siku mbili na baadaye aliruhusiwa.

Kamanda Magiligimba alisema PC Kazimir na mke wake Frola wote ni wakazi wa Mtaa wa Mitimirefu mjini hapa.

Alisema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, jambo ambalo inasadikiwa kuwa lilikuwa likiwasumbua kwa muda. Kwamba mke huyo alikuwa akimtuhumu mume wake kuwa ana ‘nyumba ndogo’.

Kamanda huyo wa polisi alisema mtuhumiwa Frola bado anaendelea kushikiliwa na kuhojiwa na baada ya uchunguzi shauri hilo litafikishwa mahakamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,987FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles