23.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

POLISI AJINYONGA KWA WIVU WA MAPENZI

Na Abdallah Amiri- Igunga

ASKARI aliyekuwa akifanya kazi katika Kituo Kidogo cha Polisi Tarafa ya Igurubi, Igunga mkoani Tabora, amejinyonga kwa kutumia shuka kutokana na wivu wa mapenzi.

Askari huyo ametambulika kwa jina la Geofrey Mwenda (32) mwenye namba G.4185. Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamisi Issa, alisema tukio hilo limetokea juzi saa tatu usiku.

Kamanda Issa alisema baada ya mke wa askari huyo kusafiri, aliamua kuwa na mpenzi wa nje ambaye hakumtaja jina lake na wakati akiendelea naye aligundua alikuwa na mwanamume mwingine.

Alisema hali hiyo ilimfanya askari huyo kuchukua uamuzi wa kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia shuka aliyoining’iniza kwenye mti.

Pia alisema askari huyo alikuwa na tabia ya kutaka kujiua mara kwa mara na akiwa katika Kituo cha Polisi cha Simbo alitishia pia kujiua kwa kunywa sumu.

Alisema akiwa Kituo cha Polisi cha Igunga pia alitaka kujiua kwa kujipiga risasi na kutokana na hali hiyo aliwataka wakuu wa vituo vyote mkoani Tabora kuwa makini pindi wanapoona kuna askari yeyote anayetaka kujidhuru.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles