24.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 8, 2024

Contact us: [email protected]

Polepole: Mwaka 2020 ni Magufuli

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, amesema kuwa alichokifanya Rais Dk. John Magufuli kwa kipindi hiki kifupi alichokaa madarakani, ni dhahiri hakuna mwingine atakayepewa ridhaa na chama zaidi yake kugombea tena urais mwaka 2020.

Polepole alitoa kauli hiyo jana Dar es Salaam, katika mahojiano na kituo kimoja cha redio.

Alisema CCM haina sababu ya kupitisha mgombea mwingine ikiwa Rais Magufuli amefanya vitu vikubwa na bado ana uwezo na nguvu ya kulitumikia taifa.

“Mwaka 2020 hatuna shaka katika nafasi ya urais mgombea wetu ni Rais Magufuli, hatuna wasiwasi kabisa na kiongozi wetu kwa aliyofanya kwa kipindi hiki, njia ni nyeupe. Lakini hatujakataza wengine kuchukua fomu, wao wachukue tu,” alisema Polepole.

Akizungumzia kupunguzwa kwa wanachama wanaotakiwa kupiga kura za maoni alisema; “Sisi hatuukatai ubaya ambao ulikuwepo zamani, tunakiri na kufuta kwa kufanya mema, CCM tuna kadi za kielektroniki, hivyo huwezi kupiga kura ya maoni kama huna kadi ile na sio kwamba tumewapunguza bali ni mabadiliko ya teknolojia, hivyo wahakikishe wanakubaliana na mabadiliko na hakuna aliyefukuzwa.”

Aidha Polepole alisema CCM haipokei tena watu wanaotoka upinzani kwa kuwa usajili umeshafungwa na kudai kuwa waliobaki hawana vigezo na wajiandae kuachia majimbo 2020.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles