29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Pogba na mapinduzi ya Mourinho Manchester United

paul-pogbaNa ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

KIUNGO wa timu ya Juventus, Paul Pogba, aliondoka Old Trafford akiwa na umri wa miaka 19 akitamani kuwa na uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza ambapo wakati huo nafasi yake ilikuwa ikichezwa na mkongwe, Paul Scholes.

Scholes aliwahi kusema kuwa hafikirii mchezaji huyo anaweza kuwa na thamani ya pauni milioni 86.

Kwa kuwa fedha hiyo inatakiwa kununua mchezaji atakayekuwa na uwezo wa kufunga mabao 50 kwa msimu kama Cristiano Ronaldo au Lionel Messi ambapo Pogba bado hajaufikia ubora wao.

Hata hivyo, Kocha Mkuu wa Manchester United, Jose Mourinho, si mjinga kumtaka mchezaji huyo kwa kiasi hicho.

Lakini swali je, Pogba ataweza kurejesha kile watu wanachotarajia kutoka kwake baada ya kununuliwa kwa gharama kubwa?

Mourinho amekuwa akitumia mfumo wa 4-2-3-1 au 4-3-3 katika kila mchezo ambao amekuwa akifanya vizuri hivi karibuni.

Katika mfumo huo, Pogba anaweza kucheza kama kiungo mshambuliaji wa uongo huku Rooney akacheza namba 10.

Pia kwa aina ya wachezaji aliowasajili utagundua kwamba ni kati ya wachapa kazi katika mifumo hiyo.

Pogba ni mchezaji anayevutia wakati wa kushambulia lango la wapinzani wakati akitimiza majukumu yake.

Anaweza kuusoma mchezo kwa haraka na kubadili aina ya mchezo kwa nguvu alizonazo ikiwa ni aina ya mchezaji ambaye alikuwa akikosekana katika timu hiyo kwa muda mrefu.

Mmoja kati ya Michael Carrick, Daley Blind au Morgan Schneiderlin, anaweza kucheza kama kiungo mkabaji, akitoa ulinzi, kupokonya mipira na kushambulia.

Pia Pogba anaweza kuongeza ladha ya kiungo anayetakiwa kucheza mtu na mtu akisaidia kusambaza mipira na kuwa sehemu kubwa ya mashambulizi ya United.

Ander Herrera amekuwa moja ya tarajio la Mourinho msimu ujao kama ambavyo kocha huyo anavyodai baada ya kufungwa na Borussia Dortmund.

“Tunataka kiungo mwenye nguvu eneo la kati kwa kuwa tunataka kushambulia hata hivyo tunatarajia kuona Manchester United yenye mabadiliko muda si mrefu lakini tunatakiwa kujituma hadi kufika katika hatua hiyo,” anasema Mourinho.

Ni mchezaji gani bora duniani zaidi ya Pogba anayeweza kufanya kama ambavyo Mourinho anavyotaka?

Toni Kroos ni mkufunzi wa kucheza na mpira akitokea eneo la kiungo anayekabia chini ya  dimba wakati Luka Modric  si kiungo wa asili hiyo kama ambavyo Pogba anavyofanya akiwa katika eneo hilo.

Kama Pogba atacheza namba 10 hataweza kuwa na nafasi ya kumpasia mshambuliaji kwa ajili ya ushambuliaji pia hataweza kushambulia.

Lakini akiwa kiungo anayekabia chini ya dimba anaweza kuipa United nafasi ya kutumia kipaji chake.

Anaweza kuwasumbua wapinzani kwa kuisumbua ngome yao na kuwafanya kutoka nje ya mchezo na kuifanya safu ya ushambuliaji ya United iwe vizuri katika shambulizi la kushtukiza.

Kwa kuwa wakati anapokuwa na mpira Pogba pia anaweza kushuti katikati ya mabeki na kubadili kasi ya ushambuliaji.

Wasiwasi kwa Manchester  ​​United utakuwa kwamba Pogba hakufanya vizuri wakati wa michuano ya Euro 2016 na alikuwa akicheza katika jukumu lile lile.

Kocha Mkuu wa Ufaransa, Didier Deschamps, alikuwa akitumia mfumo wa 4-3-3, huku Pogba akimtumia katika sehemu ya kiungo mshambuliaji wakati alipogundua  kwamba Antoine Antoine Griezmann ni nyota wa mchezo.

Griezmann aliruhusiwa kuwa huru kusogea mbele wakati wowote atakavyo wakati Pogba alilazimishwa kuwa na nidhamu zaidi na kazi kuwa ya kiungo wa chini katika mfumo wa 4-2-3-1.

Katika timu ya Ufaransa, Pogba alikuwa na jukumu kubwa zaidi ya kiungo mkimbiaji anayeweza kuwa na United inatakiwa imruhusu kufanya yake katika uwanja wakati anapoona kuna nafasi ya kufanya hivyo.

Pia kuna faida ya kuwa na mchezaji kama Pogba katika kutafuta ushindi kutokana na uwezo wake wa kupiga mashuti ya uhakika.

Mafanikio ya kiungo huyo akiwa Juventus yanatoa hamasa baada ya kushinda Ligi Kuu ya Italia, Serie A mara nne, akifanikiwa kuchukua medali baada ya Ufaransa kuibuka nafasi ya pili Euro 2016.

Msimu uliopita alikuwa kinara wa kutoa pasi za mabao katika ligi hiyo kwa kutoa pasi 12 na kufunga mabao nane katika michezo 35 ya ligi.

Mchezaji mkubwa anaweza kufanya timu ikawa bora na tayari Pogba anaonekana kuwa mchezaji wa aina hiyo.

Ni mchezaji ambaye mashabiki wa Manchester United walivutiwa naye kama ilivyokuwa kwa Paul Scholes katika misimu michache baada ya kucheza.

Hivyo klabu hiyo ilikuwa na kila sababu ya kutumia kiasi chochote ili kuhakikisha inapata saini yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles