31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

Pogba amshukuru Pirlo kumpa elimu

Paul-Pogba-JuventusTURIN, ITALIA

KIUNGO wa klabu ya Juventus, Paul Pogba, amesema anamshukuru sana kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Andrea Pirlo, kwa kumpa elimu ya kupiga mipira ya adhabu.

Pogba juzi alifanikiwa kupachika bao kwa mpira wa adhabu katika mchezo wa Kombe la Copa Italia dhidi ya Torino, ambapo Juventus ilishinda mabao 4-0, hivyo akasema ujuzi huo ameupata kwa Pirlo.

“Pirlo alikuwa ni mtu ambaye alikuwa anapenda kunifundisha kupiga mipira ya adhabu wakati tukiwa pamoja katika klabu hii, ninamshukuru sana kwa kuwa sasa naweza kufanya hivyo kama alivyonifundisha.

“Nitaendelea kumkumbuka kutokana na mambo mengi ambayo alikuwa ananifundisha, naweza kusema ameniacha katika kipindi kizuri na naweza kufanya mengi aliyoniachia,” alisema Pogba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles