24.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 29, 2023

Contact us: [email protected]

Pochettino: Nilitaka kujiua na wachezaji wangu nilipokosa ubingwa

Mauricio Pochettino
Mauricio Pochettino

LONDON, ENGLAND

KOCHA Mkuu wa timu ya Tottenham Spurs, Mauricio Pochettino, amethibitisha kwamba alitaka kujiua pamoja na wachezaji wake baada ya kukosa Ubingwa wa Ligi Kuu England  msimu uliopita, ambapo timu yake ilimaliza ikiwa nafasi ya tatu.

Spurs msimu uliopita ilionekana kuwa na kila dalili za kutwaa ubingwa huo  kabla ya kumaliza ikiwa nyuma ya Arsenal na Mabingwa Leicester City.

Matumaini ya kikosi hicho yalianza kupotea Mei mwaka huu, baada ya kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Chelsea na kujikuta ikianza kuporomoka.

Moyo wa kupambana pamoja na ari ya mchezo kwa timu hiyo viliendelea kupotea pia katika mchezo dhidi ya timu ya Southampton na Newcastle na kuwashuhudia wapinzani wao, Arsenal wakiwa juu yao.

“Nilitaka kuwaua wachezaji wote pamoja na mimi mwenyewe baada ya msimu na kujikuta tukiwa nafasi ya tatu.

“Tulipotoka ziara ya Australia wachezaji walihitaji kusikia hisia zangu, niliwaambia kama ningepata nafasi ya kuwaua ningefanya hivyo kwa kila mmoja wao pia ningejiua mwenyewe.

“Mimi ni mwaminifu kwao hata wao pia, lakini ni binadamu, ingawa ilikuwa ngumu kuendelea na wiki chache za mwisho wa msimu uliopita,” alisema Pochettino.

Kocha huyo alisema kwamba baada ya mchezo dhidi ya Chelsea ilikuwa vigumu kukabiliana na ukweli kwamba isingewezekana timu yake kuwa bingwa msimu huo.

“Sijui wachezaji wangu walikosea wapi? Hata hivyo soka ni mbinu, nguvu na ujuzi, lakini pia akili, hivyo ni vitu tunavyotakiwa kuvijua,” alisema Pochettino.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles