ZIPO taarifa mpya zinazodai uongozi wa Tottenham unaangalia uwezekano wa kumrejesha kocha wake wa zamani, Mauricio Pochettino.
Taarifa zinadai kocha wa sasa, Nuno Espirito Santo, atatimuliwa muda wowote endapo Pochettino atakubali kuiacha PSG.
Taarifa hii huenda ikapokewa kwa mikono miwili na Pochettino kwani imekuwa ikielezwa kuwa hana furaha katika klabu ya PSG.
Naye kocha aliyeko Tottenham, Nuno, anapitia wakati mgumu kwani kikosi chake kiko kwenye hali mbaya, ambapo kwa sasa kinashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.