24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

POCHETTINO AWATUMIA SALAMU CHELSEA

LONDON, ENGLAND


KOCHA wa klabu ya Tottenham, Mauricio Pochettino, amewatumia salamu wapinzani wake Chelsea kwa kuwaambia kwamba hata kama atashindwa kuchukua ubingwa msimu huu, lakini msimu ujao wajiandae.

Kocha huyo ambaye klabu yake inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi huku wakiwa nyuma kwa pointi saba dhidi ya wapinzani wao Chelsea, anaamini msimu huu amefanya makubwa na amepambana kuhakikisha timu yake inashika nafasi ya kwanza.

Pochettino amesema lengo lake msimu huu lilikuwa ni kutaka kuchukua ubingwa, lakini kutokana na ushindani anaokutana nao dhidi ya Chelsea unamfanya kujisikia vizuri, huku akiamini kama atashindwa kuchukua taji hilo msimu huu basi msimu ujao atafanikiwa.

Katika mchezo wa juzi, Tottenham ilifanikiwa kuishambulia Watford na kuifunga mabao 4-0, wakati huo Chelsea wakitembeza kichapo ugenini cha mabao 3-1 dhidi ya wapinzani wao Bournemouth.

“Kwa hali tulionayo kwa sasa, ni wazi kwamba tuna kikosi ambacho muda wote kinafikiria ushindi, hii ni nafasi nzuri kwetu kuona ni jinsi gani tutaweza kutwaa ubingwa misimu ijayo, jambo la furaha kuona wachezaji wakiwa na nidhamu ya mchezo.

“Tumekuwa tukiwapa wakati mgumu wapinzani wetu Chelsea, makosa yao ni faida kwetu, hivyo ninaamini kama tutashindwa kutwaa ubingwa msimu huu, basi tutakuwa na kikosi kizuri zaidi msimu ujao.

“Ni juu yao wenyewe kutwaa ubingwa huo, lakini ujumbe wetu ni kwamba kila mchezo tunatakiwa kushinda na sasa tunautazama mchezo unaofuata.

“Timu yetu imekuwa ikijituma tangu siku ya kwanza na sasa tunaona faida yake kutokana na nafasi tulionayo, lakini bado hatujafikia malengo yetu ila tunaamini yanaweza kufikia msimu huu au msimu ujao,” alisema Pochettino.

Michezo mingine ambayo ilipigwa juzi ni pamoja na Man City ambayo ilishinda mabao 3-1 kwenye uwanja wa nyumbani wa Etihad dhidi ya Hull City, Liverpool ikiwa ugenini ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Stoke City, West Ham wakiwatembezea kichapo cha bao 1-0 Swansea City, huku Middlesbrough ikitoka suluhu dhidi ya wapinzani wao Burnley.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles