25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 8, 2022

Contact us: [email protected]

Pluijm ashtuka, aanza kujipanga

hans-van-der-pluijmNa MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

KOCHA mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, amesema sasa yupo makini kupambana katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kushtukia ujanja unaofanywa na timu zinazoshiriki ligi hiyo msimu huu.

Yanga ambao ni wabingwa watetezi wa ligi hiyo, tayari wamecheza michezo minne na kufanikiwa kushinda mitatu huku ikilazimishwa sare mara moja.

Kocha huyo raia wa Uholanzi, aliliambia MTANZANIA jana kuwa amegundua kuwa timu zote zinakamia zaidi mechi dhidi ya Yanga, changamoto inayowalazimu kucheza mechi zote kama fainali.

Alisema ugumu wa mechi zao unatokana na sababu kwamba kila timu inapambana ili kuifunga Yanga kwa kuwa ni mabingwa, ndio maana analazimika kuongeza umakini na kuwapa wachezaji wake mbinu za ziada.

“Wapinzani wanajipanga zaidi wanapokaribia kucheza dhidi ya Yanga, maandalizi ambayo ni tofauti kabisa na yale waliyofanya katika mechi zao zilizopita, hii kwetu ni changamoto ambayo nimeanza kuifanyia kazi.

Akizungumzia mchezo wa kesho dhidi ya Stand United utakaochezwa katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Pluijm alisema anawaheshimu wapinzani wao kutokana na ubora wa kikosi walichonacho, hivyo wanajiandaa kwa mechi yenye ushindani mkubwa.

Mholanzi huyo alisema siku zote matokeo ya ushindi yanatokana na maandalizi mazuri, hivyo hawezi kubweteka kwa ushindi walioupata Jumamosi iliyopita dhidi ya Mwadui FC.

Aidha, Pluijm alisema sasa ameweka pembeni malalamiko ya ubovu wa viwanja vinavyotumika kwa mechi za ligi kuu, kwa kuwa hakuna mabadiliko yoyote yanayoweza kufanyika kubadilisha hali hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,682FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles