Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Kampuni ya Plascon imesema imejipanga kutatua changamoto ya mfuriko jijini Dar es Salaam kwa kutengeneza mabomba yanayokidhi miundombinu.
Hayo yamesemwa juzi na, Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Plasco Ltd inayozalishaji wa mabomba, Alimiya Othuman amesema kampuni yao inayozalisha mabomba ya weholite yanayotumika katika miundombinu ya barabara na maji.
Amesema wamejipanga kuondoa kero ya mafuriko katika Jiji la Dar es Salaam kwa kuweka mambo maalumu yenye uwezo wa kutunza maji kipindi cha mvua zinaponyesha.
“Kwa sasa tunazalisha mabomba ya kisasa na yenye ubora wa kimataifa, chagamoto tunazozipata kwa sasa ni kuwepo kwa makampuni yanayozalisha mabomba kutoka nje ya nchi na kuyaingiza nchini ambayo yako chini ya kiwango ukilinganisha na mabomba yetu, lakini pia wao wamekuwa wakilipa kodi kidogo tofauti na tunayolipa sisi,” amesema Othuman wakati wa ziara ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbli waliotembelea kiwanda chao kilichopo Chang’ombe Dar es Salaam na akujionea shughuli za uzalishaji unavyoendelea.