30 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Pipi zamponza waziri wa elimu Madagascar

ANTANANARIVO, MADAGASCAR

WAZIRI  wa elimu nchini Madagascar amefukuzwa kazi kwa sababu ya mipango yake ya kuagiza pipi zenye thamani ya zaidi ya dola milioni 2 sawa na (£1.6m) kwa watoto wa shule.

Waziri huyo, Rijasoa Andriamanana alisema wanafunzi watapewa pipi tatu kila mmoja watakazokula baada ya kunywa dawa ya mitishamba inayodaiwa kutibu virusi vya corona nchini humo ambayo bado haijathibitishwa.

Mpango huo ulitupiliwa mbali baada ya kupingwa na Rais Andry Rajoelina wa Madagascar.

Rais Rajoelina anapigia debe dawa ya mitishamba walioibaini kama yenye uwezo wa kutibu virusi vya corona.

Nchi kadhaa za Afrika zinaendelea kuagiza dawa hiyo ya mitishamba inayoaminiwa kusaidia katika kukabiliana na virusi vya corona lakini Shirika la Afya Dunia (WHO) limeonya kuwa dawa hiyo bado haijathibitishwa kuwa na uwezo huo.

Taasisi ya Taifa ya Matibabu nchini Madagascar pia nayo imetilia shaka uwezo wa dawa hiyo inayotokana na mmea wa pakanga yaani (Artemisia) ikisema kwamba inaweza kusababisha matatizo ya afya kwa watu.

Rajoelina alisema kama taifa la ulaya lingetengeneza dawa, mapokeo yangekuwa ya tofauti

Rais Rajoelina amepuuzia ukosoaji juu ya dawa hiyo ya mitishamba, akisema ni wazi kuwa nchi za magharibi inadharau uwezo wa Afrika.

“Kama ingekuwa ni nchi ya Ulaya ambayo imegundua dawa hii, Je kungekuwa na mashaka kiasi hiki, Sidhani,” aliambia chombo cha habari cha Ufaransa cha France 24.

Karibia watu 1,000 wamethibitishwa kupata virusi vya corona nchini humo, pamoja na vifo saba ambavyo vinahusishwa na virusi hivyo.

Hatua za kutotoka nje pia zimewekwa lakini Rais Rajoelina amekosolewa vikali kwa jinsi alivyokabiliana na janga hilo nchini humo.

Mapema wiki hii kulitokea vurugu katika mji uliopo mwashariki mwa nchi hiyo wa Toamasina, ambapo wanajeshi wamepelekwa eneo hilo kuhakikisha raia wanatekeleza hatua za kukabiliana na corona zilizowekwa na wizara ya afya.

Chanzo cha ghasia hizo ni mchuuzi wa barabarani aliyepigwa na vikosi vya usalama. 

Hata hivyo maofisa wamekanusha madai ya kutekeleza vurugu za aina yoyote ile.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,352FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles