29.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 19, 2022

Pinda: Watanzania kuweni na hofu ya Mungu

Walter Mguluchuma-Katavi

WAZIRI Mkuu mstaafu Mizengo Pinda amewataka Watanzania kujenga misingi ya imani ya kidini ili kwenda sambamba na maendeleo yaliyopo nchini.

Pamoja na hali hiyo alionya kuwa hatua ya kuwapo kwa ongezeko la idadi ya watu inaweza kuwa ni hatari ya nchi ikaingia katika mmomonyoko wa maadili, ikiwa jamii haitajengwa na kuwa na hofu ya Mungu.

Hayo aliyasema jana wakati wa ibada ya Jumapili katika Parokia Kuu ya Mtakatifu Maria Imakulata, Jimbo Katoliki la Mpanda, alipokuwa akitoa salamu kwa waumini wa kanisa hilo.

Alisema kwa sasa maendeleo ya nchi yameongezeka kutokana na ongezeko la idadi ya watu ambao kwa sasa wanakadiriwa kufikia milioni 55 hadi 56.

“Hivyo idadi hiyo ya watu na maendeleo ya nchi lazima yaendane na Wanzania kujengwa katika imani za kidini ili kuiepusha nchi isije kuingia kwenye mmomonyoko wa maadili kama zilivyo nchi nyingine za Amerika,” alisema Pinda.

Hata hivyo, alionya juu ya athari za utandawazi ambazo zimekuwa kubwa hapa nchini na duniani jambo linalosababisha watu kuishi bila kuwa na imani na hofu ya Mungu kama ilivyo katika baadhi za nchi za Amerika.

Aliwaomba waumini wa kanisa hilo kutohuzunika kwa kuhamishwa kwa askofu wao, Gerevansi Nyaisonga, ambaye amekuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Mbeya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,987FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles