26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Pinda: Tuwe tayari kupokea matokeo yoyote ya uchaguzi

Anna Potinus

Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda amewataka Watanzania kuwa tayari kupokea matokeo yoyote yatakayopatikana baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Ametoa kauli hiyo leo leo Jumanne Oktoba 29 alipokuwa akifungua kongamano la kitaifa la kudumisha amani na usalama kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, amesema kila mmoja anapaswa kuheshimu ushindi huo kwani unatokana na kudra za Mwenyezi Mungu.

“Nchi yetu ni muhimu zaidi kuliko maslahi yetu binafsi na ningependa mfahamu kuna maisha kabla na baada ya uchuguzi, na ninaamini serikali imeshakamisha maandalizi yote ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu,”.

“Kila mmoja wetu awe tayari kupokea matokeo yoyote, kumpokea mgombea yeyote atakayeshinda na kuheshimu ushindi huo kwani unatokana na kudra za Mwenyezi Mungu,”.

“Tanzania inajivunia kama kisiwa cha amani barani Afrika kwa takribani miaka 50 hivyo sisi kama wananchi hatuna budi kuilinda kwani bila amani hakuna kitu kinachoweza kufanyika,” amesema Pinda.

Aidha amesema kila rai ana haki ya kulinda amani ya nchi kwa kutoa taarifa pale anapoona kuna kikundi chochote chenye lengo la kuivunja amani ya nchi hiyo na kuachana na imani kuwa kazi hiyo ni ya serikali pekee.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles