26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Pili kunogesha kitchen party Gala kwa vyakula vya uswahilini

BEATRICE KAIZA

Msanii wa vichekecho nchini, Gladness Kifaluka ‘Pili’ ametambulisha rasmi vyakula vya uswahilini ‘PiliGallina’ akishirikiana na ‘KitchenpartyGala’

Akizungumza na Mtanzania Digital jana, alisema kuwa vyakula vya uswahilini ni msosi ambao unapendwa na watu wengi ila wanashindwa kuvipata sehemu zuri na yenye usafi ndio maana ameona ni vema kuwapa mashabiki zake kile kitu roho inapenda na vyakula hivyo vitakuwa ninapatikana ‘BuscarlaVida’.

“Vyakula vya uswahilini miguu ya kuku, utumbo, shingo na vingine yote unavipata kutoka kwa PiliGallina kwa bei nafuu,” alisema Pili.

Aidha alitoa shukrani zake kwa timu zima ya ‘KichenpartyGala’ kwa kuweza kuona alicho nacho na kumpatia fursa ya kuwa sehemu ya kuwapa chakula kitamu.

Kwa upande wake muandaaji wa shughuli hiyo ambaye ni mtangazaji wa kituo cha redio, Dina Marious alisema kuwa Kitchen party Galla ya mwaka huu ambayo kauli mbiu ni ‘Raha za Uswahili itafanyika Oktoba 18, mwaka huu kuanzia saa 5:00 asubuhi katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles