PICHA ZA UTUPU ZA BLAC CHYNA ZALETA KIZAAZAA

0
999

NEW YORK, MAREKANIMWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, Blac Chyna, anatarajia kumpeleka mahakamani baba wa mtoto wake, Rob Kardashian, kutokana na kutishia kuachia picha zake za utupu.

Wawili hao ambao mapema mwaka huu walifanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza, imeripotiwa kuwa wameachana, hivyo Rob Kardashian ametishia kuachia mitandaoni picha za utupu za mama wa mtoto wake.

Kutokana na kitendo hicho, Blac ameweka wazi kuwa anatarajia kwenda mahakamani ili kumshtaki Rob kwa kitendo ambacho ametishia kukifanya.

“Rob kaa tayari kwenda mahakamani kwa kitendo unachotaka kukifanya, sina muda wa kugombana kila mmoja anafanya mambo yake, kwa upande wangu nafanya kile ambacho ninajisikia kukifanya, nina fedha za kutosha kufanya nitakalo,” aliandika Black.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here