25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Picha| Waziri Dk. Kijaji aongoza wadau kutembelea banda la Brela mkoani Tanga

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji, akipata maelezo juu ya huduma tunazozitoa kwenye maonesho ya Tisa ya Biashara na Utalii kutoka kwa Afisa Leseni wa BRELA, Saada Kilabula. Maonesho haya yameanza Mei 28, 2022 mkoani Tanga. BRELA inawahamasisha wananchi kutembelea banda lake ili kupata huduma mbalimbali.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abdallah, akipata maelezo ya namna Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), inavyotoa huduma zake kwenye Maonesho ya Tisa ya Biashara na Utalii leo Mei 30, 2022 wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho hayo, kwenye uwanja wa Mwahako mkoani Tanga.
Afisa Tehama Msaidizi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Hillary Mwenda(kulia) akitoa usaidizi wa usajili wa Jina la Biashara kupitia mfumo wa usajili kwa njia ya Mtandao (ORS) kwa, Emmanuel Mallya((aliyesimama) kutoka Korogwe mkoani Tanga kwenye Maonesho ya Tisa ya Biashara na Utalii yanayofanyika katika Uwanja wa Mwahako mkoani Tanga. Katika maonesho hayo BRELA pia inatoa huduma za Usajili wa Kampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma, kupata Leseni ya Kiwanda, Leseni ya Biashara kundi A, kupata Hataza na kutoa mafunzo pamoja na usaidizi juu ya kutumia mfumo wa ORS.
Afisa Usajili kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Julieth Kiwelu(kulia) akitoa elimu ya Hataza kwa, Musini Abdallah katika Maonesho ya Tisa ya Biashara na Utalii yanayofanyika katika Uwanja wa Mwahako mkoani Tanga. Katika maonesho hayo BRELA pia inatoa huduma za Usajili wa Kampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma, kupata Leseni ya Kiwanda Leseni ya Biashara kundi A, na mafunzo pamoja na usaidizi juu ya matumizi ya mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS).
Msajili Msaidizi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Selemani Selemani akitoa usaidizi kwa, Hafsa Kwallow juu ya namna ya kujaza katiba ya kampuni kwenye Mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS) kwenye Maonesho ya Tisa (9) ya Biashara na Utalii yanayofanyika katika Uwanja wa Mwahako mkoani Tanga hadi tarehe 6 Juni, 2022. Katika maonesho hayo BRELA inatoa huduma za Usajili wa Kampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma, kupata Leseni ya Kiwanda, Leseni ya Biashara Kundi A, kupata Hataza na kutoa mafunzo na usaidizi juu ya matumizi ya mfumo wa ORS.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles