22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Picha| PSPTB yawakaribisha Wananchi kutembelea banda lake Sabasaba

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Dk. Alban Mchopa, akikabidhiwa zawadi na Meneja Masoko na Uhusiano wa Bodi hiyo, Shamim Mdee(wapili kulia) baada ya kupata maelezo ya huduma zinazoendelea kwenye banda hilo Julai 6, 2022 kwenye maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(SABASABA). wengine wanaoshuhudia ni watumishi wa bodi hiyo.
Picha ya pamoja ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi(wa kwanza kulia) akiwa pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Charles Mnyeti(watatu kutoka kulia) na Dk. Alban Mchopa(watatu kutoka kushoto) wakiwa na watumishi wa PSPTB kwa ajili ya maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA).

Banda la Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) lipo ndani ya jengo la Wizara ya Fedha na Mipango ambapo pia inatoa huduma ya kuhuisha taarifa, elimu ya jinsi ya kujisajili kwa ajili ya Mitihani ya PSPTB na Uanachama kwa njia ya mtandao.

Hivyo, Bodi hiyo imewahimiza Watanzania mbalimbali kutembelea banda hilo kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali zinazohusiana na fani hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles