PHARRELL WILLIAMS AMPIGA MKWARA TRUMP

0
1517

NEW YORK, MAREKANI


STAA wa muziki nchini Marekani, Pharrell Williams, amempiga mkwara rais wa nchi hiyo kwa kitendo chake cha kutumia wimbo wake wa ‘Happy’ bila ya ruhusa yake.

Inasemekana kuwa, wimbo huo ulisikika ukipigwa kwenye mkutano baada ya mauaji ya Sinagogi ya Pittsburgh huku ikidaiwa watu 11 walipoteza maisha.

Mwakilishi wa msanii huyo amedai wimbo huo ni hakimiliki ya Pharrell Williams, hivyo hauwezi kupigwa bila ruhusa yake kama ilivyofanyika.

Mbali na Williams, wasanii wengine ambao wametoa onyo kama hilo ni pamoja na Adele, Queen, Prince na wengine wengi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here