NEW YORK, MAREKANI
MKALI wa muziki wa Hip Hop nchini, Pharrell Williams, amesema ataendelea kuonekana kijana kutokana na jinsi anavyoitunza ngozi yake.
Msanii huyo mwenye umri wa miaka 44, amesisitiza kuwa ataendelea kuonekana kijana kutokana na kufuata ushauri wa wataalamu wa ngozi.
“Kwa sasa umri wangu ni mkubwa, nina miaka 44, lakini naonekana tofauti na wengine ambao wana umri kama wangu, nadhani hii inatokana na jinsi mwenyewe unavyotaka kuonekana.
“Nitaendelea kuonekana hivi kutokana na kufuata ushauri wa wataalamu wa ngozi jinsi ya kutumia aina ya mafuta na vyakula, bila wao nadhani mwonekano wangu usingekuwa nilivyo sasa,” alisema Pharrell.