26.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 24, 2021

PETROLI YASHUKA, DIZELI, MAFUTA YA TAA YAPAA

Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM


MAMLAKAya Udhibiti wa Huduma za Nishati na  Maji Tanzania (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei ya petroli huku dizeli na mafuta ya taa vikipanda kwa wastani wa Sh saba hadi 12 kwa lita moja.

Bei hiyo ni tofutti ikilinganishwa zilizotangazwa Machi Mosi mwaka huu.

Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi   Dar es Salaam  jana ilieleza kuwa bei hiyo itaanza kutumika rasmi hii leo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa bei ya rejareja ya petroli imepungua kwa Sh tatu kwa lita moja sawa na asilimia 0.13, huku bei ya jumla ikishuka kwa Sh 5.65 kwa lita au asilimia 0.29.

Wakati petroli ikishuka, bei ya dizeli imepanda kwa Sh 12 kwa lita moja sawa na asilimia 0.63, bei ya jumla imeongezeka kwa Sh 9.11 kwa lita sawa na asilimia 0.50.

“Bei ya rejareja ya mafuta ya taa imepanda kwa Sh saba kwa lita sawa na asilimia 0.36 ambako bei ya jumla imepanda kwa Sh 3.68 kwa lita sawa na asilimia 0.21.

“Kwa kiasi kikubwa, mabadiliko haya ya bei yametokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia, mfumuko wa bei na gharama za usafirishaji (BPS Premiums) ikilinganishwa na mwezi uliopita,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

 Ilisema Machi mwaka huu hakuna mzigo wa mafuta uliyopokelewa nchini kupitia bandari ya Tanga.

“Ongezeko hilo la bei za mafuta linatokana na ongezeko la faida ya wauza mafuta wa jumla na rejareja kutokana marekebisho yaliyofanywa kukidhi matakwa ya mfumko wa bei kwa mujibu wa kanuni ya ukokotoaji wa bei za mafuta katika mwaka 2016,” iliongeza taarifa hiyo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,967FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles