23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Petra Muzic: Rapa Mkenya mwenye mpango wa kusaidia wasichana kielimu

*Baada ya Dimpoz, awavuta G Nako, Joh Makini

CHRISTOPHER MSEKENA

KATIKA ukanda huu wa Afrika Mashariki, kuna idadi ndogo sana ya wasanii wakike wanaofanya muziki wa Hip hop kwa ukubwa unaostahili. Bado haijajulikana kwanini lakini waliopo wamefanikiwa kupenya na kujitengeneza mashabiki lukuki.

Mwaka 1995, huko pwani ya Mombasa, Kenya alizaliwa Petra Bockle, mrembo kutoka familia ya mama Mkenya na baba mwenye asili ya visiwa vya Seychelles ambaye kwenye muziki tunamtambua kama Petra Muzic, rapa aliyefanya unyama wa hatari, kwenye kolabo yake mpya na Ommy Dimpoz, One & Only.

Nikurudishe nyuma mpaka mwaka 2018, ambapo rapa mahiri Khalighaph Jones, alimtupia mrembo huyo kwenye kolabo yao Rider, ngoma iliyovuma katika ukunda huu wa Afrika Mashariki na wapenzi wa Hip hop, wakaendelea kuupa vyeo uwezo binafsi wa Petra Muzic katika kurap, mitindo na uandishi wa mistari konki.

Hivi karibuni, Petra Muzic ambaye ni mke na mama wa mtoto mmoja, alitembelea ofisi za gazeti hili na kupiga stori na mhariri wa Swaggaz, mazungumzo ambayo yalilenga kumpa nafsi ya kuendelea kujitambulisha kwa mashabiki zake wapya, maisha na mengineyo mengi, karibu.

Swaggaz: Kwanini umeamua kufanya Hip hop na siyo muziki mwingine kama ambavyo wanafanya warembo wengine?

Petra Muzic: Naweza kusema ni kipaji, mimi naweza kufanya vitu vingi kama kupiga ngoma, kuimba kidogo ila nimechagua kufanya muziki wa Hip hop.

Swaggaz: Msanii gani wa Hip hop alikushawishi ufanye unachofanya na kwanini?

Petra Music: Eminem, sababu ni mtu ambaye anaishi maisha yake kama mtu wa kawaida na ana kile kipaji cha asili ambacho Mungu amempa na huwa najiona niko kama yeye.

Swaggaz: Ilikuwaje rapa mkubwa kama Khaligraph Jones kukupa kolabo?

Petra Muzic: Mimi na Khaligraph tumejuana muda mrefu kabla hajawa staa na kwangu amekuwa King wa Hip hop siku zote toka kitambo.

Tulianza muziki pamoja ila mimi nikaacha sababu tasnia ya muziki ya Kenya ni tofauti na Bongo kule wakisikia wewe ni noma wanakuzima.

Kwa hiyo yeye aliendelea mimi nikachukua likizo ili niangalie mambo ya familia na mtoto. Kuna siku tulikutana kwenye kazi akaniambia kwende studio tukafanye kitu mnoma sana, ndiyo ikatokea ile ngoma Rider ambayo hata mama yangu anaipenda.

Swaggaz: Mpango wako wa kusaidia elimu kwa wasichana hapa Afrika Mashariki umeishia wapi?

Petra Muzic: Bado upo mimi nipo sana kwenye hizi kampeni za kusaidia watoto wakike, kuwainua wanawake na masuala ya kijinsia, kuna mradi nipo nao nikishirikiana na Brighter Communities Worldwide.

Tumepanga kutambulisha ‘Application’ ya simu ambayo itakuwa inaunganisha wadhamini dunia nzima ambao watakuwa wanaweza ‘ku-adopt’ (kuasili) msichana kutoka kwenye hiyo ‘App’.

Kwa hiyo mdhamini atapakua ‘App’ na atakutana na hao wanafunzi wasichana wenye changamoto kupitia shule zao, jambo ambalo litafanya msaada wa kielimu umfikie mhusika moja kwa moja.

Kwasababu kuna shida kubwa sana Kenya na nchi zote za Afrika Mashariki, unakuta msichana anakosa shule kwasababu hana taulo za kike, watu wengi wanafanya ikiwamo serikali lakini kumekuwa na skendo za wizi, unakuta fedha zimeibiwa ila kwa hii ‘App’ utakuwa unaingia tu kama unavyoingia Instagram, kwahiyo kwa mdhamini itampunguzia matatizo ya kutuma hela bila kujua inakwenda wapi.

Swaggaz: Turudi kwenye muziki, Watanzania wengi wamekufahamu baada ya kufanya wimbo na Ommy Dimpoz, mlikutana vipi mpaka mkafanya kazi?

Petra Muzic: Nilikutana na Ommy Dimpoz naye akiwa kwenye  ziara ya kutambulisha wimbo wake Yanje kule Kenya, alikuwa bado mgonjwa, tulikutanishwa na mtangazaji maarufu wa Kenya, Shaffie Weru,  aliinita nikaenda, tukakutana na tukapanga namna ya kufanya na wimbo, tukaingia studio chini ya prodyuza wa Sauti Sol, One & Only ukatokea.

Swaggaz: Baada ya Ommy Dimpoz kuna kolabo zingine umefanya na wasanii wa Bongo?

Petra Muzic: Kolabo zipo, kuna G Nako lakini pia nimefanya kazi na Joh Makini, inatoka hivi karibuni ni wimbo mzuri wa kujibizana yaani ‘battle to battle’ siyo ngumu sana, kila mtu anaweza kusikiliza ni wimbo wa klabu.

Swaggaz: Rapa gani wakike wa Tanzania unapenda kazi zao?

Petra Muzic: Mimi huwa sichangui jinsia sababu mimi mwenyewe nikifanya ngoma huwa sijiangali kama msichana, huwa naangalia nani ni msanii mkali kwahiyo nawafuatilia wote wanaofanya vizuri.

Swaggaz: Karibu tena Tanzania.

Petra Muzic: Shukrani sana, nimewapenda Watanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles