29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Petr Cech atangaza kustaafu soka

LONDON, ENGLAND

MCHEZO wa fainali ya juzi ya Kombe la Europa, ulikuwa wa mwisho kwa mlinda mlango namba moja wa Arsenal, Petr Cech, ambaye amedai anastaafu soka.

Katika fainali hiyo, Chelsea ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 na kutwaa ubingwa huo, hivyo kipa huyo alisema ni mchezo wake wa mwisho katika soka la kulipwa.

Januari mwaka huu kipa huyo aliweka wazi kuwa mwishoni mwa msimu huu atatangaza kustaafu soka, hivyo mchezo huo wa juzi ulikuwa wa mwisho kwa timu hizo kucheza soka msimu huu. Cech aliwahi kuwa mlinda mlango wa Chelsea tangu mwaka 2004 hadi 2015 alipojiunga na Arsenal.

Wiki kadhaa zilizopita kulikuwa na taarifa kwamba, baada ya mchezaji huyo kutangaza kustaafu soka atarudi katika klabu yake ya zamani ya Chelsea na kuwa mkurugenzi wa timu na si mchezaji.

“Najivunia mimi mwenyewe kwa kiwango nilichokionesha kwenye mchezo huo bila ya kujali matokeo tuliyoyapata, ukipata nafasi ya kucheza mchezo wa mwisho katika maisha yako ya soka ni kitu cha kujivunia.

“Siwezi kujutia chochote kilichotokea kwenye soka langu, ninaamini nimefanya kile ambacho nilikuwa ninastahili kukifanya. Tulipambana kwa kila namna kwa msimu wote lakini hatujafanikiwa. Ila ninaamini msimu ujao timu hii itakuwa bora zaidi.

“Kwa sasa mimi ni mchezaji wa Arsenal hadi pale mkataba wangu utakapomalizika Juni 30 mwaka huu, niliweka wazi kuwa huu utakuwa ni mchezo wangu wa mwisho, hivyo sina kitu cha kuongeza kikubwa ni kusubiri Juni 30 ifike,” alisema kipa huyo.

Katika kipindi chake cha soka, mlinda mlango huyo amefanikiwa kutwaa jumla ya mataji 16, tangu alipoanza kucheza soka la kulipwa mwaka 1999, huku akiwa amecheza jumla ya klabu tano katika maisha yake ambazo ni Chmel Blsany, Sparta Prague, Chelsea na Arsenal.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles