Na Wandishi Wetu
Simba imeanza kuliamsha baada ya leo kumsainisha mkataba wa miaka mitatu mchezaji aliyekuwa anasubiriwa kwa hamu na Wanamsimbazi, Peter Banda raia wa Malawi kutoka timu ya Big Bullet.
Banda anacheza nafasi ya kiungo, lakini ana uwezo wa kumudu sehemu nyingine ikiwamo ushambulaji.
Nyota huyo anakuwa wa kwanza kusajiliwa na Simba kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/22.
Kwa mujibu wa taarifa ya klabu ya Simba, wamepanga usajili wa kisayansi ili kuboresha kikosi huku dhamira ya kwanza ikiwa ni kutetea ubingwa pamoja na kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.