22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

PETER AKANUSHA P-SQUARE KUVUNJIKA

LAGOS, NIGERIA

NYOTA wa muziki anayeunda kundi la P-Square, Peter Okoye, amekanusha taarifa za kuvunjika kwa kundi hilo.

WIKI iliyopita kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii nchini Nigeria, zilienea taarifa kwamba wawili hao wamegombana na kila mtu anaamua kufanya kazi binafsi.

“Naomba kuweka wazi kuwa, hakuna ukweli wowote juu ya P-Square kuvunjika, tunashangazwa na taarifa hizo zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii.

“Wengi wamekuwa na wasiwasi kwa kuona katika baadhi ya kazi zangu natumia jina la Mr P, hii haina maana kwamba kundi limevunjika, ila nimeamua kutumia jina hilo kwa kuwa nina watoto mapacha, hivyo kuna kitu kinakuja kwa ajili yao na ndio maana nimeamua kutumia Mr P, lakini kundi lipo pale pale na kazi zinaendelea kuja,” alisema Peter.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,283FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles