Pete ya ndoa Nicki Minaj usipime

0
1325

NEW YORK, MAREKANI

RAPA Nicki Minaj, ameianika pete ya ndoa yake na kuweka wazi kuwa alitumia kiasi cha dola milioni 1 kuinunua, ambapo ni zaidi ya bilioni mbili za Kitanzania.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 36, wiki moja iliopita alianika taarifa kuwa amefunga ndoa na mpenzi wake Kenneth Petty, lakini ndoa hiyo ilikuwa ya kimya kimya.

Juzi wawili hao walitumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kuionesha pete hiyo ya almasi ikiwa imetengenezwa kwenye kampuni maalumu ya Raffaello, ambapo ilichukua miezi kadhaa kubuni pete hiyo.

Ndani ya pete kuna maneno yakisomeka Ken na Barbie. Hata hivyo baada ya kuposti picha huyo kampuni iliotengeza pete hiyo ilikuwa ya kwanza kuwapongeza kwa kufanikisha kufunga ndoa yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here