24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Pesa za Zawadi NMB MastaBata zabaki Mil. 100

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital 

MSIMU wa Tatu wa Kampeni ya NMB MastaBata inayoendeshwa na Benki ya NMB, umezidi kushika kasi kuelekea ukingoni baada ya Alhamisi Machi 3, kufanyika kwa droo ya tisa, ambako washindi 100 walijinyakulia Sh. Milioni 10, hivyo kufanya pesa zilizopata washindi kufikia Sh milioni 140 kati ya Sh milioni 240 zinazoshindaniwa.

Ofisa  Kitengo cha Kadi Benki ya NMB, Lightness Zablon, akibonyeza kitufe cha kompyuta kumtafuta mmoja kati ya washindi 100 wa droo ya tisa ya Kampeni ya ‘NMB MastaBata Kivyako Vyako’ iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Ofisa Huduma kwa Wateja, Suzan Manga na kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Elibariki Sengasenga.

NMB MastaBata – Kivyako Vyako, ni kampeni inayohamasisha matumizi na manunuzi kwa njia ya kadi badala ya pesa taslimu, ambayo inaendeshwa kwa kipindi cha wiki 10, zitakazoshuhudia wateja 1,080 wakijishindia pesa taslimu Sh milioni 240, wakiwamo washindi 1,000 wa wiki, washindi 50 wa mwezi na 30 wa ‘Grande Finale.’

Akizungumza kabla ya uchezeshwaji wa droo hiyo jijini Dar es Salaam, Ofisa wa Kitengo cha Kadi wa NMB, Lightness Zablon, alibainisha kuwa kampeni hiyo imekuwa na mafanikio makubwa, kwani imeongeza idadi ya miamala ya matumizi kwa njia ya kadi za MasterCard, Mastapass QR, vituo vya Mauzo (PoS) na mtandaoni.

“Tayari wateja 850 wamejishindia zawadi ya pesa taslimu katika wiki nane zilizopita, pamoja na droo mbili za mwisho wa mwezi Januari na Februari. Na leo tunaenda kupata washindi wengine 100 wa wiki ya tisa, hivyo tumebakisha wiki moja (washindi wengine 100) na droo ya fainali ya washindi 30 mwishoni mwa mwezi huu.

“Kampeni imeonesha mafanikio makubwa kwa kuwa imeongeza idadi ya miamala. Maana yake ni kwamba mwitikio wa matumizi ya kadi umekuwa mkubwa, kulingana na mahitaji ya kidijitali, ambako sasa unaweza hata kuagiza bidhaa nje ya nchini na kulipia kwa njia za kadi, badala ya pesa taslimu ambazo ni hatari kwa usalama,” alisema.

Droo hiyo ilifanyika chini ya uangalizi wa Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Elibariki Sengasenga, ambaye aliwahakikishia wateja wa benki hiyo kwamba kampeni hiyo inafanyika kwa kufuata vigezo, kanuni na sheria zinazotambulika na bodi yake na kuwatoa shaka wateja juu ya upatikanaji washindi.

Wakati washindi 100 wa kila wiki wakijishindia Sh 100,000 kila mmoja, washindi 25 wa droo ya mwisho wa mwezi wa NMB MastaBasta hujishindia Sh. Milioni 1 kila mmoja, huku washindi 30 watakaopatikana kwenye ‘grande finale’ wakitarajia kujinyakulia Sh milioni 3, hivyo washindi 1,080 watazoa Sh milioni 240.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles