23 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

PERU YAMTAKA TRUMP KUMSALIMISHA RAIS TOLEDO

LIMA, PERU

RAIS wa Peru, Pedro Pablo Kuczynski, ametoa wito kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, kumsalimisha Rais wa zamani wa hapa Alejandro Toledo anayetakiwa kujibu mashitaka nchini hapa.

Toledo, ambaye inaaminika kwa sasa yupo mjini San Francisco, Marekani anatuhumiwa kupokea rushwa ya dola milioni 20, tuhuma ambazo amezikana.

Kupitia njia ya simu juzi, Kuczynski alimwomba Trump ‘kutathmini’ hali hiyo.

Kufikia sasa, juhudi za kumkamata Toledo zimekwama kutokana na changamoto za kisheria.

Marekani imesema haiwezi kumkamata kiongozi huyo wa zamani hadi maelezo zaidi kuhusu kesi inayomkabili iwasilishwe kwake na maafisa wa Peru.

Maafisa nchini Peru, ambao waliomba akamatwe wiki iliyopita, wanahofia kwamba huenda akaondoka Marekani na kwenda Israel.

Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel ilisema haitamruhusu Toledo kuingia nchini humo hadi ‘masuala yanayomhusu nchini Peru yatakapohitimishwa.

Toledo, ambaye kwa sasa ni profesa mwalikwa katika Chuo Kikuu cha Stanford nchini Marekani aliiongoza Peru kuanzia 2001 hadi 2006.

Anatuhumiwa kupokea rushwa kutoka kwa Kampuni ya Ujenzi ya Odebrecht ya Brazil ili kuisaidia kupata kandarasi ya kujenga barabara kuu ya kuunganisha Peru na Brazil.

Zawadi ya dola 30,000 imeahidiwa yeyote atakayetoa habari zitakazosaidia kukamatwa kwa Toledo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles