Pep Guardiola rasmi Manchester City

0
525

pep_2111869aManchester, Uingereza

KLABU ya soka  ya Manchester City imethibitisha kumpa mkataba wa miaka mitatu kocha wa timu ya Bayern Munich, Pep Guardiola (44).

Hatua hiyo imekuja baada ya kocha wa timu hiyo, Manuel Pellegrin kuthibisha kuwa atafungasha vilago mwishoni mwa msimu huu.

Guardiola anatarajia kuanza kibarua chake kipya Julai Mosi mwaka huu huku timu hiyo ikitajwa kuwapiku baadhi ya timu zilizokuwa zikinyemelea saini ya kocha huyo.

Kwa mujibu wa chanzo kutoka kwenye klabu hiyo, Manchester City itakuwa imewapiku wapinzani wao, Manchester United   na Chelsea.

Desemba mwaka jana Guardiola  alitangaza kwamba angeondoka Bayern Munich  mwishoni mwa msimu huu licha ya kutothibitisha  angetimkia wapi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here