20.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Pep Guardiola akubali kujiunga Juventus

TURIN, ITALIA

KOCHA wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini England, Manchester City, Pep Guardiola, amefikia makubaliano na uongozi wa klabu ya Juventus kwa ajili ya kuisimamia timu hiyo kwa mkataba wa miaka minne.

Inadaiwa kwamba, kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri, anatarajia kuondoka mara baada ya kumalizika kwa msimu huu ili kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine, hivyo kwa mujibu wa mwandishi kutoka nchini Italia, Luigi Guelpa, ameweka wazi kuwa tayari Juventus wamekubaliana na Guardiola.

Guelpa amedai kuwa habari hizo ni za uhakika kwa kuwa amezipata kwa chanzo cha habari ambacho kilimpa taarifa juu ya Cristiano Ronaldo kutaka kuondoka Real Madrid na kujiunga na Juventus.

“Nimepata habari za uhakika kwamba Guardiola amefikia makubaliano na Juventus kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo kwa mkataba wa miaka minne ijayo, taarifa hiyo nimeipata kwa mtu ambaye aliniambia kwamba Ronaldo anakwenda kujiunga na Juventus,” alisema mwandishi huyo.

Guardiola ambaye mkataba wake unatarajia kumalizika mwishoni mwa msimu wa 2021, ameweka historia ya kutwaa Ligi Kuu nchini Hispania, Ujerumani na England, hivyo kuna uwezekano wa kwenda Italia kwa ajili ya kuendeleza historia yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,595FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles