23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Pep Guardiola ajisalimisha mapema

MANCHESTER, ENGLAND

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, ameanza kujisalimisha mapema kutokana na ushindani wa Ligi Kuu nchini England huku akisema hawezi kuwa bingwa kila msimu.


Kocha huyo amesema hata kwenye mchezo wa gofu na tenisi mabingwa huwa wanapoteza, hivyo hata yeye kwenye soka kuna msimu anaweza kukutana na ushindani wa hali ya juu na akashindwa kufanya vizuri.


Nafasi ya Manchester City kutetea ubingwa msimu huu ni ndoto kutokana na ushindani uliopo, timu hiyo kwa sasa inashika nafasi ya kwenye msimamo wa Ligi baada ya kucheza michezo 13 na kujikusanyia pointi 28, wakati huo Leicester City wakiwa na pointi 29 nafasi ya pili huku Liverpool wakiwa vinara kwa pointi 37.


Manchester City imeachwa pointi tisa na wapinzani hao Liverpool, hivyo Guardiola anaamini anaweza hasifanye vizuri msimu huu, ilo ni jambo la kawaida kwenye michezo ya aina yoyote.


“Presha kubwa iliopo kwa sasa kwenye timu yetu ni kuhofia kushindwa kutetea ubingwa, lakini hili ni jambo la kawaida kwenye mchezo wa aina yoyote, siku zote ushindani unakuwa mkubwa na tunapambana ili kuhakikisha tunatimiza lengo letu.


“Bingwa wa mchezo wa gofu hawezi kushinda kila wakati, hata mabingwa wa tenisi pia wanapoteza, hivyo hata mimi ninaweza kupoteza kwa kuwa michezo ndiyo ilivyo, ila tunapambana kuhakikisha tunatetea ubingwa, bado tuna nafasi kwa kuwa ligi bado ipo nyuma, lakini wapinzani wetu na wao wanapigania nafasi ya ubingwa,” alisema Guardiola.


Mabingwa hao watetezi wamekuwa na wakati mgumu msimu huu kutokana na baadhi ya wachezaji wake kuwa majeruhi tangu mwanzo wa msimu, lakini kuna taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo kuwa baadhi ya wachezaji wake wameanza kufanya mazoezi mepesi kwa ajili ya kutaka kurudi viwanjani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,411FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles