27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

PENDEKEZO LA ‘KUMZAWADIA’ KENYATA UWAZIRI MKUU LAZUA MJADALA KENYA

NAIROBI, KENYA


PENDEKEZO la kuunda wadhifa wa waziri mkuu kwa ajili ya Rais Uhuru Kenyatta wakati atakapostaafu limeibua mjadala mpya kuhusu kampeni ya mabadiliko ya Katiba.

Bosi wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi Kenya (Cotu), Francis Atwoli alichochea mjadala huo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mjini hapa juzi.

Atwoli alidai Uhuru bado yu kijana na hivyo hapaswi kuachwa astaafu wakati muhula wake wa sasa wa pili na wa mwisho utakapofika kikomo.

Uhuru ana miaka 55 na atakuwa na 59 wakati atakapomaliza muda wake madarakani mwaka 2022.

Pendekezo la kiongozi huyo wa Cotu linafanana na mfumo wa Urusi, ambao ulimshuhudia Rais Vladmir Putin na Waziri Mkuu Dmtry Medvedev  wakibadilishana nyadhifa huko nyuma.

“Hebu tubadili Katiba hii na kuchukua muswada wa Bomas ili kupambana na utengaji, kwa kutambua kuwa si wote tunaoweza kuwa rais. Hii itaturuhusu kuendelea kufurahia mchango wa Rais Uhuru Kenyatta, ambaye ni kijana sana. Vinginevyo wapi tutampeleka?” alihoji Atwoli.

Muswada wa Katiba wa Bomas unapendekeza kuhamisha sehemu kubwa ya madaraka ya rais kwa waziri mkuu anayechaguliwa na Bunge.

Kiongozi wa upinzani, ambaye alihudhuria maadhimisho hayo kwenye viwanja vya Uhuru, Raila Odinga, hakutoa maoni yoyote kuhusu kauli ya Atwoli.

Odinga ambaye pia amekuwa akiupigia chapuo muswada wa Bomas, aliishia kusema tu kuwa makubaliano ya amani na mshikamano baina yake na Uhuru hayazuiliki.

Naibu Rais William Ruto amekuwa mara kwa mara akipinga mpango wa mabadiliko ya Katiba kuunda nyadhifa mpya.

Spika wa Bunge la taifa, Justin Muturi na viongozi wa wengi Bungeni Aden Duale na Seneta Kipchumba Murkomen waliponda tamko hilo la Atwoli.

Walisema ijapokuwa kila Mkenya ana haki ya kuzungumzia suala hilo, mabadiliko hayapaswi kuwa kwa ajili ya kumhifadhi mtu fulani.

Aidha Duale alikumbishia Rais Kenyatta ameshaweka wazi kuwa atafurahi kustaafu akimaliza muhula wake.

“Iwapo Atwoli anatafuta ajira kwa baadhi ya watu, anapaswa kusema wazi na aache kutumia jina la Rais,” Duale alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles