27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

Pellegrini: Mimi ni kocha sahihi West Ham

LONDON, ENGLAND

MBALI na timu ya West Ham kukubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Arsenal, juzi kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, kocha wa timu hiyo Manuel Pellegrini, amedai bado yeye ni mtu sahihi wa kuisimamia timu hiyo.


West Ham walikubali kichapo hicho kwenye uwanja wa nyumbani mabao yakifungwa na Gabriel Martinelli, Nicolas Pepe na Pierre Aubameyang, jambo ambalo limemfanya kocha huyo kuendelea kuwa katika wakati mgumu wa kulinda kibarua chake.


Lakini kocha huyo anaamini mbali na kuchezea kichapo bado ana nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko ya matokeo hayo.


“Tuliweza kuumiliki mchezo kwa dakika 60, sikushangazwa na kitendo cha mashabiki kuzomea kwa kuwa hatujaweza kushinda hapa kwa michezo mitatu, najua kama utakosa matokeo kwenye uwanja wa nyumbani lazima mashabiki watakosa furaha, inaumiza kwa kuwa timu ipo chini inashika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa Ligi.


“Akili yangu inawaza kubadilisha matokeo na ninaamini uwezo huo ninao, hivyo mashabiki waamini hilo kila kitu kitakuwa sawa,” alisema kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles