LEJENDARI wa soka nchini Brazil, Pele, amesema anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondosha uvimbe wa koo.
Pele, mchezaji pekee kuwahi kuibeba mara tatu ‘ndoo’ ya Kombe la Dunia, ana umri wa miaka 80 na aliwahi kuzichezea klabu za Santos na New York Cosmos.
Mkongwe huyo alifanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Albert Einstein iliyoko mjini Sao Paulo na alitarajiwa kuruhusiwa leo.
Hivi karibuni, ilielezwa kuwa Pele anakabiliwa na msongo wa mawazo uliosababisha apoteze fahamu, jambo ambalo aliibuka na kulikanusha.