PBPA yabadili masharti ili wazawa kuagiza mafuta

0
762
Kituo cha Petroli Puma
Kituo cha Petroli Puma
Kituo cha Petroli Puma

Na Joseph Lino,

Waswahili husema mcheza kwao hutunzwa na mtu kimfaacho chake na hivyo Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) nchini imetangaza neema kwa kampuni za ndani  kwani zinatarajiwa kupewa fursa katika zabuni ya uagizaji wa  bidhaa za mafuta kwa pamoja baada ya kutangaza kuanza kutoa kipaumbele kwa kampuni hizo kuanzia January mwaka kesho.

Kilio cha makampuni ya ndani kimesikika na wahusika na hivyo kusababisha mabadiliko ambayo yataleta tija kwao na nchi kwa ujumla.

Hatua hiyo imekuja baada ya kampuni za ndani kutoshiriki katika uagizaji huo tangu uliponza mwaka 2012 kutokana na gharama kubwa za uagizaji na vigezo  vilivyowekwa kuwa muhali  kwa wengi na hivyo kampuni hizo zilishindwa kuvitimiza.

Kwa muda mrefu kampuni za nje za Sahara……ya …na Addax Agusta…ya …zilikuwa zikishinda zabuni kutokana na uwezo wao kifedha, lakini kwa kuwa hivyo serikali na nchi ilikuwa inapata hasara ya kukosa kodi ya mapato ya biashara hiyo.

Akizungumza na MTANZANIA jijini Dar es Salaam juzi Mkurugenzi wa PBPA, Micheal Mjinja, alisema taratibu mpya za utoaji zabuni zimebadilika hivyo kampuni za ndani zitapewa kipaumbele katika mchakato huo kwa kubadilisha masharti na mwenendo wa biashara.

“Tumebadilisha vigezo kutokana na malalamiko ya makampuni  ya ndani hasa kiasi cha fedha kilichohitajika kilikuwa kikubwa ambapo walikuwa hawawezi,” alisema Mjinja.

Kwa maelezo ya PBPA, zabuni ya mafuta ilikuwa inatolewa kwa miezi miwili miwili ambapo ilikuwa inahitaji kiasi kikubwa  cha fedha kwa taratibu za sasa na hivyo kubadili kuanzia mwezi huu.

“Kwa sasa zabuni itakuwa inatolewa kwa mwezi mmoja mmoja, ambapo imepunguza gharama kwa kiasi kikubwa, na hivyo kuvutia wengi”

Pia alifafanua, “Tumeamua tuondokane na mshindi mmoja kuchukua mafuta yote kwa pamoja, ila tunaanza zabuni ya kila meli. Hapo tutakuwa tumepunguza uwingi wa mafuta na kampuni nyingi za ndani zitashiriki, na hivyo kuongeza ushindani ”.

Sio hivyo tu kwani hata bidhaa nyingine za mafuta zimejumuishwa ili kupata soko lililo sawa kwa wote.

Kwa upande wa kampuni za nje alisema serikali imeamua kuwa  makampuni yote ya nje ili waweze kushinda zabuni wanatakiwa kujisajili hapa nchini  ilikutimiza haja kuanzia Januari mwakani.

“Zabuni kuwa zinatolewa kwa makampuni ya nje ambao hawalipi kodi hapa, mwakani inabidi wasajiliwe Tanzania ili kodi ipatikane,”

Kwa maelezo ya PBPA, thamani moja ya meli moja ya mafuta dizeli inafikia takribani dola za marekani milioni 45 au 48 kwa meli yenye ujazo wa tani 80,000 hadi100,000.

Kwa upande wa petroli meli moja inakuwa ujazo wa kati ya tani 36,000 hadi 38,000.

Kwa bei ya wiki iliyopita mafuta kwa  metriki tani moja ilikuwa dola za Kimarekani 480 hadi 490  kwa mafuta ya dizeli ambapo mafuta ya petroli yalikuwa 450 hadi 460 kwa metriki  tani, kwa maelezo ya PBPA.

“Kwa namna hii makampuni yatakayoshiriki tunarajia yataongezeka, kwa  kuwa  tumepunguza vigezo na hivyo kuzidisha ushindani .

Mkurungezi huyo alifafanua  na kuasa kuwa ili makampuni ya ndani yaweze kushinda  kirahisi washirikiane na mabenki mbalimbali ili kupata uwezo wa kifedha kwani biashara yenyewe inalipa na kukopesheka.

“Katika mchakato huu, kunahitajika  suala la fedha  nyingi ambazo ni mabenki yakipewa nafasi ya kutoa fedha kwa makampuni ya ndani wanaweza kufaulu  kushinda zabuni kama watajizatiti kama ilivyokuwa hapo awali kabla haijakuwepo PBPA”.

Mafuta yakishaingia nchini kampuni za usambazaji na masoko huchukua mgao wao na kuuza kwa rejareja kwa wenye vituo vya mafuta na kugawa nchi nzima.

PBPA ni wakala wa kuagiza mafuta nje ya nchi kwa kutumia kampuni mahsusi za shughuli hizo ambazo zimejisajiri nayo kwa kufanya biashara hiyo kwa mfumo wa zabuni kwa kila mwezi kwa kila kampuni kutoa bei anayoweza kuleta mafuta hayo na mara nyingi yule mwenye bei ndogo ndiye hushinda ingawa katika mazingira maalumu  wakati fulani mwenye bei kubwa ndiye aliyeshinda zabuni.

Hili limekuwa ni eneo mojawapo ambapo  TRA kwa niaba ya serikali ilikuwa inapoteza mapato mengi ya kodi na hasa ikizingztiwa kuwa mafuta ndio bidhaa inayochukua takribani nusu ya mapato ya fedha za kigeni kuyaagiza kutoka nje.

PBPA imeboresha miundo mbinu ya kudhibiti mapato kwa kutengeneza mita inayosoma kiasi kinachoingia nchini na hivyo kuzuia manya kupoteza mapato ya serikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here