22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Pazia la Euro 2016 kufunguliwa leo

Euro 2016 drawPARIS, UFARANSA

MICHUANO ya Kombe la Euro 2016, inatarajia kuanza kutimua vumbi leo nchini Ufaransa huku timu 24 zikiwania taji hilo.

Michuano hiyo itapigwa kwa siku 30 huku viwanja 10 vikitarajia nyasi zake kutibuliwa kutokana na mikiki mikiki hiyo.

Wenyeji wa michuano hiyo timu ya Taifa ya Ufaransa watashuka dimbani leo hii wakipambana na Romania kwenye Uwanja wa Saint-Denis. Leo utakuwa ni mchezo wa ufunguzi kwa timu hizi mbili, lakini kesho michezo mitatu itapigwa kwenye viwanja tofauti.

Katika michuano hii kuna wachezaji ambao wanatazamwa sana kwa ajili ya kuzisaidia timu zao akiwamo nyota wa klabu ya Real Madrid, ambaye alikuwa kwenye nafasi ya pili ya mchezaji bora wa dunia katika Tuzo za Ballon d’Or mwaka jana, Cristiano Ronaldo.

Nyota huyo anapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwa ajili ya kujiweka sawa katika kuwania tuzo hiyo ya dunia, huku akikiongoza kikosi chake cha timu ya Taifa ya Ureno ambapo kinaonekana kuwa vizuri baada ya kushinda mabao 7-0 dhidi ya Estonia katika maandalizi ya Euro huku Ronaldo akifunga mabao mawili.

Wakati huo, Gareth Bale, mchezaji ghali kuliko wote duniani naye akitegemewa kung’ara na nchi yake ya Wales. Washindi wa Kombe la Dunia 2014, Ujerumani wao watakuja na majina kadhaa kama vile mlinda mlango wa Bayern Munich, Manuel Neuer, mshambuliaji Thomas Muller na kiungo wa Real Madrid, Toni Kroos.

Wafaransa watang’arishwa na kiungo wa Juventus, Paul Pogba ambaye kwa sasa anaangaliwa na klabu mbalimbali za Ligi Kuu barani Ulaya katika kipindi hiki cha usajili.

Ubelgiji hawako nyuma, watakuwa na Eden Hazard na Kevin de Bruyne wakati Sweden ikimwangalia nyota wake, Zlatan Ibrahimovic.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles