Paulin Zongo, Kimobitel, Joan kurudi upya

Pauline Zongo 7NA MWALI IBRAHIM

KUNDI la Ndege watatu linaloundwa na wanamuziki watatu; Paulin Zongo, Hadija Mnoga ‘Kimobiteli’ na Joan Matovolwa, linatarajia kujitambulisha tena kwa mashabiki wake kwa kuachia wimbo mpya wa ‘Mr Mapromise’.

Kimobitel alisema wameamua kurudi kivingine wakiwa wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanatoa burudani ya kutosha kwa mashabiki wao.

“Sasa hivi wote tupo huru hatuna bendi nyingine tunazozitumikia, hivyo tunataka kuliinua kundi letu na kuanza mashambulizi rasmi,” alisema.

Kimobitel alisema tayari wameshakamilisha nyimbo mbili ambazo ni ‘Misukosuko ya mapenzi’ iliyofanyiwa video na ‘Wanawake tunaweza’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here