29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

PASS Trust yazindua kampeni ya Kijanisha

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS Trust) imezindua kampeni ya Kijanisha Maisha na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo mkoani Singida kwa kuhamasisha uzalishaji unaozingatia ukuaji wa kijani shirikishi ili kuongeza tija katika sekta ya kilimo.

Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa social training center, mkoani Singida, wamejadili njia za kuharakisha na kuimarisha maendeleo endelevu ya kiuchumi kwa kutilia mkazo Ajenda ya Ukuaji wa Kijani Shirikishi kwa kilimo endelevu kitakachotosheleza mahitaji ya kujikimu, kibiashara na kuhakikisha usalama wa chakula cha uhakika na kilimo stahimilivu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo katika mkutano huo, Meneja wa maendeleo ya biashara wa PASS Trust, Herman Bashiri amesema,

“PASS Trust ina mchango mkubwa katika kuchochea na kuwezesha ukuaji wa kilimo nchini Tanzania huku tukitoa kipaumbele kwa vijana na wanawake ambapo tunawapa dhamana ya mikopo na huduma za maendeleo ya biashara ili kufikia malengo yao,” amesema Bashiri.

Aidha ameongezea kuwa Wakulima wananufaika na PASS Trust kwa kuwekewa dhamana ya mikopo ya kilimo, mifugo na uvuvi kupitia benki mbalimbali nchini.

“Tunatoa dhamana ya hadi asilimia 80 ya mikopo kwa wakulima, wavuvi, wafugaji na wenye viwanda wanaozalisha kwa kufuata kanuni za uhifadhi wa Mazingira na kupitia kampuni yetu tanzu ya PASS Leasing piaa tunawezesha upatikanaji wa zana za kilimo,” amesema.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba ametoa pongezi kwa PASS Trust juu ya kuja na mpango wa kukuza uchumi kupitia ajenda ya Ukuaji wa Kijani Shirikishi.

“Naipongeza PASS Trust kwa ubunifu na kuanzisha ajenda ya Ukuaji wa Kijani Shirikishi ambayo kwa hakika inachochea maendeleo endelevu ya kiuchumi ambayo yanaenda sambamba na utunzaji wa mazingira na kuongeza tija katika uzalishaji wa kilimo,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles