25.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Parimatch yazinufaisha timu za Tanzania

Mwandishi wetu

Kampuni ya michezo ya Kubahatisha ya Parimatch Tanzania leo Alhamisi Agosti 20, imetimiza azma ya kusaidia timu zenye uhitaji muhimu zilizoweza kushiriki katika kinyang’anyiro cha shindano la ‘Amsha Ndoto’ ambalo linaendeshwa kisasa mtandaoni kwa kuwapatia jezi, mipira na vifaa vingine vya kufanyia mazoezi.

Shindano hilo ambalo lilizinduliwa rasmi Julai 21 mwaka huu jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa Parimatch Tanzania, Tumaini Maligana na kuzitaja timu hizi kuwa ni Lifofo fC inayotokea Kawe, Bonyokwa fC iliyopo Tabata Segerea, Tambaza ya Kariakoo pamoja na Ilala United ya jiji la Dar es Salaam.

Maligana amesema kuwa Parimatch imejengwa katika misingi ya kusaidia jamii na kwamba Kampeni ya Amsha ndoto ni miongoni mwa sehemu ya kurudisha kupitia eneo la michezo.

“Tunafahamu michezo ni nguzo muhimu za burudani na afya hususani kwa vijana lakini pia kwa uendelevu wake, michezo ni ajira pia na ndio maana tukaamua kujikita katika timu ambazo hazipo katika daraja lolote zenye ndoto ili kusudi waweze kujiajiri kupitia michezo.

“Sisi kama Parimatch kwa uwezo tuliokuwa nao tutaweza kufanya kila liwezekanalo ili kuamsha ndoto za vijana zitimie na huu ni mwanzo tu lakini tutakapoona wadau wengine wa michezo wanaungana nasi katika hili basi hii Amsha Ndoto itakuja kuwa ni kitu kikubwa sana,” amesema Maligana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,454FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles