26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Parimatch wajitosa kuibeba Mbeya City

NA BEATRICE KAIZA

KAMPUNI ya Michezo ya Kubahatisha ya Parimatch Tanzania, leo imeingia rasmi mkataba wa kuidhamini Mbeya City inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao (2020-21).

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa Parimatch Tanzania, Tumaini Maligana, amesema mkataba huo ni faida kwa klabu hiyo si tu katika ligi, bali kwenye michuano mingine itakayoshiriki.

“Tunaamini kuwa mwanzo huu utafungua milango ya ushirikiano na klabu na ligi zingine ambazo Parimatch inadhamini kimataifa,” amesema Maligana.

Ameongeza kuwa walipanga kuanza na klabu yenye ushawishi, hivyo wakaona Mbeya City ina kigezo hicho. “Mbeya City ni Klabu kubwa kwa hapa Tanzania, hususan ukiangalia idadi ya mashabiki. Parimatch ni kampuni inayohudumia na kujali watu wote ingawa tumeanza na Mbeya City,” amesema.

Wakati huo huo, Maligana amemtaja mshindi wa tuzo ya bao bora kwa msimu uliopita wa Ligi Kuu, Paston Shikala, akisema amewavutia pia kupeleka udhamini wao Mbeya City.

“Baada ya kuona lile goli la Paston Shikala ambalo ndilo bora kwa msimu (uliopita), nasi tukaona huku ni kuzuri. Tutaenda kwa vilabu vingine pia, iwe Ligi Kuu au Ligi Daraja la Kwanza, ikiwa ni kuunga mkono juhudi za TFF na Bodi ya Ligi katika kuhakikisha ligi za Tanzania zinakuwa na tunaenda kimataifa,” anasema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles