23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

PARESO ‘AKINUKISHA’ BUNGENI

Na Fredy Azzah, Dodoma

Mbunge wa Viti Maalumu, Cecilia Pareso (Chadema), ameitaka serikali kupeleka bungeni marekebisho ya katiba ili nchi irudi kwenye mfumo wa chama kimoja kutokana kuminywa kwa vyama vya upinzani.

Pareso amesema hayo leo alipokuwa akichangia kwenye Hotuba ya Makadrio na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ambapo pamoja na mambo mengine, amesema kwa sasa chaguzi ndogo zimeonyesha kuwa vyama vya upinzani vinasimama dhidi ya polisi badala ya chama kingine cha siasa.

Amesema pia imekuwa kawaida kwa viongozi wa upinzani sasa kukamatwa kila wakati ama kutakiwa kuripoti polisi hivyo wengi wana kesi nyingi huku mikutano ya hadhara vyama vya siasa ikipigwa marufuku.

“Waasisi wetu walituaminisha kuwa tuna maadui watatu, ujinga maradhi na umasikini, lakini sasa hivi mmeongeza adui mwingine ambaye ni vyama vya upinzani.

“Mimi nawashauri mlete mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba ili dunia ijue kuwa sisi tuko kwenye mfumo wa chama kimoja na mridhike,” amesema Pareso.

Pamoja na mambo mengine, Pareso amedai pia kutokana na viongozi wa upinzania kuhamia kwenda  chama tawala ambapo hadi sasa imetumisha Sh bilioni 6.9 kwenye chaguzi za marudio wakati Bunge lilitenga Sh bilioni nne tu za uchaguzi wa marudio pale itakapotokea kifo kwa mmoja wa wawakilishi waliochaguliwa.

Wakati Pareso akichangia, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, aliomba kutoa taarifa na kusema; “polisi wapo kwa ajili ya kulinda raia na mali zao wakati wa uchaguzi na wakati usio wa uchaguzi.”

Amesema pia takwimu zinaonyesha Chadema wasiposhiriki uchaguzi huwa hakuna fujo ila wakishiriki hali hiyo hutokea na hivyo, serikali haiwezi kuvumilia kuona raia wanakatwa mapanga na kutekwa.

Akijibu taarofa hiyo, Pareso alimtaka Mwigulu kwasababu anaingia katika Baraza la Mawaziri basi amwambie Rais  John Magufuli afute vyama vya upinzani nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles