23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Papa wa zamani adai kuna wanaotaka kumnyamazisha

VATICAN, ITALY

KIONGOZI wa zamani wa Kanisa Katoliki, Papa mstaafu Benedict wa 16 amewatuhumu wapinzani wake kutaka kumnyamazisha wakati akishambulia kwa lugha kali ndoa za jinsia, kupitia kitabu kipya kilichoidhinishwa kuhusu maisha yake kilichochapishwa jana Jumatatu nchini Ujerumani.

Papa huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 93 ambaye jina lake la kuzaliwa ni Joseph Ratzinger alidai kwamba katika maisha yake kama Benedict wa 16 alikuwa muhanga wa upotoshaji wa makusudi wa hali halisi, katika hatua alizochukuwa kuingilia kati katika mijadala ya imani ya Kanisa. 

Hayo yalibainishwa katika vipengee vya kitabu hicho vilivyochapishwa na vyombo vya habari Ujerumani na shirika la habari la DPA. 

Ilielezwa kwamba kiongozi huyo wa zamani wa Kanisa Katoliki duniani, Benedikti wa 16 alisema yu radhi kutoweka wazi sababu haswa, kwa nini watu wanataka kuinyamazisha sauti yake. 

Kanisa Katoliki nchini Ujerumani kwa miaka limekuwa likiongozwa na viongozi wa dini hiyo wanaotaka zaidi mageuzi kuliko misimamo mikali ya utamaduni wa Kanisa unaofungamanishwa na Ratzinger.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,460FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles