Papa kuruhusu wanaume waliooa kuwa mapadri

0
793

VATICAN, ITALIA

MAASKOFU wa Kanisa Katoliki wamepiga kura kuruhusu wanaume waliooa kuwa mapadri katika eneo moja la pembezoni mwa Amazon ambalo linakabiliwa na upungufu wa makasisi. 

Hatua hiyo imekuja baada ya Kiongozi wa kanisa hilo, Papa Francis kutoa ombi la kutoa ruhusa kwa wanaume walioa kuwa mapadri kwenye sehemu maalum katika eneo hilo la Amazon.

Ombi hilo la Papa limekuja baada ya waamini wa eneo hilo kuwaona kwa nadra mapadri wakati mwingine baada ya miezi au hata miaka.

Kwa sasa Papa anaruhusu wanaume walioa kuwa mapadri katika makanisa ya mashariki ya kati pekee.

Upigaji kura unafikia ukingoni huko Vatican kutokana na uhaba wa mapadru ili mapendekezo hayo yaanze kufanya kazi rasmi.

Kura zimechukuliwa kwa kipindi cha wiki tatu,kwa maaskofu 180 wa mjini Rome.

Wakiwa wanaangalia majukumu ya wanawake katika kanisa na namna mazingira yatakavyoweza ruhusu.

Papa Francis amesema yeye na washiriki wengine wanaojulikana kama ‘synod’ wapo wazi kwa mawazo ya kutafuta njia mpya itakayosaidia kusambaza imani hiyo.

Kutokana na ombi  hilo watahitajika kupata wanaume wanaoheshimika na kulingana na stakhabadhi hizo watafanya kazi katika jamii wanazotoka.

Maaskofu wa Marekani Kusini wamekuwa wakipigania juhudi hizo ili kukabiliana na upungufu wa mapadri katika eneo hilo.

Lakini wakosoaji wamedai kuwa Papa anapaswa kuhamasisha mapadri wasioe, ingawaje katika karne ya kwanza ya kanisa, mapadri waliruhusiwa kuoa, na karibia mapapa wote wa mwanzo walikuwa wameoa.

Vilevile imeelezwa kuwa kuruhusu wanaume walioa katika sehemu za Amazon ambazo zinakabiliana na ukosefu wa mapadri, kutaenda kinyume na sheria za kikatoliki ambazo zimekuwepo kwa miaka kadhaa sasa.

Kanisa katoliki ni taasisi kongwe ya kidini ambayo imekuwa na historia kwa zaidi ya miaka 2000 iliyopita huku ikiwa na mabilioni ya waumini.

Inakadiriwa karibu 85% ya vijiji huko Amazon haviwezi kusherehekea Misa kila wiki kwa sababu ya uhaba huu na wengine huonana na makuhani mara moja tu kwa mwaka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here